Slider[Style1]

HABARI

BONGO MOVIES

BONGO FLEVA

.

BONGO VIDEOS

Style5[ImagesOnly]

STORY ZA INSTAGRAM

JAJA,MSUVA KUNG'AA KWENYE MECHI YA NGAO YA JAMII UWANJA WA TAIFA LEO

Jaja aliingia ‘mzima mzima’ pembezoni mwa lango la Thika kuhakikisha anaiunganishia nyavuni krosi ya Msuva kwa vyovyote na akafanikiwa akimuacha kipa Mganda, Hamza Muwonge anaokota mpira nyavuni. Kwa furaha ya bao hilo, Jaja ambaye alikuwa akizomewa na mashabiki wa Simba SC kila alipokosea alitoka nje ya Uwanja kushangilia bao hilo, kwa shangwe za aina zote alizoweza. Yanga SC haikucheza vizuri kipindi cha kwanza na zaidi ilitegemea kupitisha mashambulizi yake pembeni walipokuwa wakiteleza kwa awamu Simon Msuva, Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho. Coutinho alikaribia kufunga mara mbili kwa mipira ya adhabu aliyopiga kutoka nje kidogo ya eneo la penalti, wakati Jaja hakuwa na madhara kabisa kipindi cha kwanza. Nafasi nzuri zaidi kwa Thika ilikuwa dakika ya 20 wakati shuti la Moses Odhiambo lilipodakwa na kipa Deo Munishi ‘Dida’- zaidi ya hapo, safu ya ulinzi ya Yanga SC leo ilicheza vizuri. Kipindi cha pili, kocha Mbrazil Marcio Maximo alianza na mabadiliko katika safu ya kiungo akimpumzisha Hassan Dilunga na kumuingiza Hamisi Thabit, ambaye alikwenda kuibadilisha timu.
 
 
Simon Msuva 
 Mchezaji jaja kutoka kwenye timu ya yanga footbal club awa mchezaji nyota baada ya kuichapa timu ya rambramba Azam Fc bao mbili yeye mwenyewe uku baadae mchezeji Nyota wa Yanga Fc Simon Msuva kutundika bao la mwisho yani la tatu kwa wapinzani wao hao

mabovu story.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram , Twitter Na Facebook

YANGA SPORTS CLUB KUIVAA AZAMA FC LEO TAIFA

 KIKOSI KAZI CHA YANGA FC
KIKOSI KAZI CHA AZAM FC
NGAO YA JAMII
mabovu story.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram , Twitter Na Facebook

Alichosema Cristiano Ronaldo baada ya Falcao kuhamia Man United

IMG_6950.JPG
Usiku wa jana klabu ya Manchester United ilikamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao kwa mkopo.
Falcao ambaye alikuwa akiwindwa na vilabu vya Arsenal na Man City amejiunga na Man U akitokea klabu ya Monaco ambayo alijiunga nayo akitokea Atletico Madrid.
Usajili wa mchezaji umezungumzia na watu wengi mmoja wao ni mchezaji bora wa ulaya na dunia – Cristiano Ronaldo.
Akiongea jijini Madrid Ronaldo alisema: ‘Falcao ni mchezaji mzuri sana, nadhani Manchester United wamefanya jambo zuri kumsajili. Sidhani kabisa kama ni mchezaji asiyewafaa, ni mchezaji wa daraja la dunia na hivyo naamini huu usajili mzuri.”

Unaambiwa Man United wamekamilisha usajili mwingine wa huyu Muargentina.

IMG_6524.JPG
Baada ya usajili wa Ander Herrera na Luke Shaw, Manchester United wamekamilisha usajili wa mchezaji mwingine ambae ni Marcos Rojo, beki wa kiargentina aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Sporting Lisbon.
Rojo ambaye alichaguliwa katika kikosi bora cha kombe la dunia, amejiunga na United kwa ada ya uhamisho wa £16 pamoja na Luis Nani kwenda Sporting kwa mkopo ambapo pia Manchester United wanaripotiwa kuhamishia nguvu zao kwa Angel di Maria wa Real Madrid.

Usajili wa Luis Suarez FC Barcelona na rekodi mpya ya gharama za usajili

20140711-165857-61137370.jpg
Baada ya uwepo wa tetesi za kuihama Liverpool kushika hatamu kwa takribani wiki 3 sasa, hatimaye leo hii Luis Suarez amejiunga rasmi na FC Barcelona akitokea Liverpool.
Usajili wa Suarez umeigharimu FC Barcelona kiasi cha £65m kwa mujibu wa mtandao wa Barcelona, na hii ni rekodi kwa Liverpool – Suarez anakuwa mchezaji aliyeuzwa kwa fedha nyingi zaidi na klabu hiyo iliyoshika nafasi ya pili kwenye EPL msimu uliopita.
Suarez ambaye alijiunga na Liverpool akitokea Ajax, pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji anayeshika nafasi ya nne kwa kusajiliwa kwa fedha nyingi zaidi nyuma ya Bale, Ronaldo na Neymar.
20140711-173034-63034421.jpg
Hata hivyo pamoja na usajili huo mchezaji huyo hatoweza kuitumikia Barca mpaka adhabu yake ya kufungiwa mechi 8 na kifungo cha miezi 4 kitakapoisha.

Cheki mapenzi ya shabiki huyu mwenye umri mdogo kwa mchezaji Neymar

n
Ukizungumzia taifa ambalo limetoa mastar kadhaa wa soka Duniani hutoacha kulitaja Brazil hii ni kufuatia rekodi zake kadhaa ambazo limewahi kujiwekea kwenye medali ya soka duniani leo limeingia kwa headline tena taifa hili.
Ni kuhusu mtoto mdogo amabye kwa kumtazama anaweza kuwa na umri usiozidi miaka 3,amekua ni miongoni kati ya walioumizwa na taarifa za kidaktari zinazomhusu mchezaji Neymar kuwa hatocheza mechi nyingine za Kombe la Dunia.
dogo 
Kama unakumbuka Neymar alipata majeraha baada ya kuumia kwenye mechi iliyochezwa kati ya Brazil na Colombia na katika mechi hiyo Brazil ilifanikiwa kushinda goli 2-1 na kufanikiwa kuingia nusu Fainali.
nnnnJuly 08 Brazil ambao kimsingi ndio wenyeji wa mashindano haya ya kombe la dunia itacheza na Ujeruman,mchezo utakaochezwa bila Neymar katika mechi ya Nusu Fainali.

Timu ya Algeria imerudi nyumbani kutokea kombe la dunia, hapa kuna picha 5 za jinsi walivyopokelewa

algeria 2
Kwenye kombe la dunia linaloendelea nchini Brazil, Algeria kutoka Afrika wameingia kwenye headlines zenye rekodi za kudumu kutoka kwenye mashindano haya baada ya kuwa moja ya timu mbili za Africa zilizogusa kwenye hatua nzuri kabla ya kutolewa.

Algeria 
Tayari timu hii imerejea nyumbani Afrika ambapo kiukweli imepokelewa kwa shangwe sana, na naamini hata wengine wasio Waalgeria wangeipokea timu kama hii kutokana na ilichofanya.
algeria 3 

algeria 4 

algeria 5 

Algeria 

Kuhusu kundi la wahalifu linalouza tiketi za kombe la dunia kinyume cha sheria Brazil.

ticketsJeshi la polisi nchini Brazil limesema kuwa linawashikilia watu 11 ambao wametengeza kundi linalojihusisha na uuzaji wa tiketi za kombe la dunia kinyume cha sheria.
Mtandao huo unadaiwa kuwa limejipatia fedha kinyume cha sheria kwa kuuza tiketi na tayari wamefanya uhalifu huo katika viwanja vinne vya kombe la dunia.
Baadhi ya tiketi hizo zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya wadhamini wakati nyingine zikiwa zimewekwa kwa ajili ya maafisa wa timu ya Brazil.
Polisi wanaamini kuwa baadhi ya tiketi zimeuzwa kwa watalii wa kigeni.

WHEAT CLICK THIS PHOTO