Slider[Style1]

HABARI

BONGO MOVIES

BONGO FLEVA

.

BONGO VIDEOS

Style5[ImagesOnly]

STORY ZA INSTAGRAM

Utamaduni wa kujiweka makovu Afrika

Kutia alama mwilini umekuwa utamaduni kwa miongo kadhaa katika maeneo tofauti barani Afrika ili kuashiria urithi wa kikabila.
Vitendo hivi hata hivyo vinapungua lakini bado kuna watu wanaotaka kuendeleza kilichofanya na mababu zao.
Katika mji wa Ouidah kaskazini mwa Benin, kuna tambiko inayotarajiwa kufanyika ikifuatwa na siku mbili za sherehe.
Houeda ni mojawapo wa makabila nchini Benin inayoamini kuwa tendo la kuchanja watoto – hasa usoni- huwaunganisha na mababu zao.
Watoto hao hupewa majina mapya, wananyolewa vichwa vyao na kupelekwa katika makazi ya watawa ambapo kuna mizimu inayowasaidia kuzungumza na vizazi vya hapo awali.
'Utamaduni unaoenziwa'
“Hii ni sehemu ya tamaduni zetu na ni muhimu sana kwangu,” anasema Genevieve boko, ambaye mwanawe wa kike mwenye umri wa miezi 6, Marina, pamoja na wapwa zake Luc na Hospice wenye umri wa miaka 10 na miaka 12 wote wako tayari kuchanjwa.
Jivu hutumika kutia alama sehemu ambayo chanjo hiyo hufanywa na huchukua sekunde chache chanjo hiyo kufanya.
“Rafiki zangu waliniuliza iwapo ni uchungu na iwapo nililia na nikasema ‘la!’,” alisema Luc baadae. “Kabla, nilipokuwa nikitembea mitaani pamoja na ndugu yangu mkubwa aliye na makovu, watu hawangeamini kuwa ni ndugu yangu. Sasa nina furaha kwa kuwa tunafanana.”
Tangu mume wake alipoaga dunia, Gamba Dahoui amekuwa akifanya chanjo zote za nyumbani-anasafisha vifaa vya kuchanjia kwa mimea yenye dawa pamoja na tembo. Makaa pia huwekwa kwenye majeraha ili kuyasaidia kupona.
Dahoui hutumia kisu kimoja tu kila wakati, huku akipuuza mashari rasmi ya kutumia nyembe safi kwa kila mtu ili kuepuka hatari ya kuambukiza magonjwa yanayoambukizwa kwa damu kama vile pepopunda na UKIMWI.
Chanjo hizi hata hivyo zimeanza kupoteza umaarufu. Idadi kubwa ya familia inashiriki sehemu ya kwanza tu ya sherehe hizo, na kuacha kabla ya chanjo kufanywa.
Ni sawa sawa na sehemu mbalimbali ya taifa hilo ambapo kila kabila huwa na mfumo wake wa kuchanja.
'Ni aibu kukosa alama au makovu'
“Nikiwa na makovu yangu, ninatambulika kila mahali ninapokwenda,” anasema Fleury Yoro, anayeishi Atacora, kaskazini mwa taifa hilo. “Iwapo ningepata nafasi ya kufanya uamuzi, singependa kuwekewa makovu namna hii.”
Anasema kuwa alipokuwa akisoma katika jiji kubwa zaidi nchini Benin Cotonou, alikejeliwa mara kwa mara kutokana na makovu yake. Watu kadhaa ‘‘hawangependa watu wengine wadhani kuwa walikuwa marafiki na mtu mshenzi namna ile,” anasema.
Wengine wana maoni tofauti ya kufanya uamuzi wa kutochanja vizazi vichanga. Sinkeni Ntcha aliacha kitendo hicho baada ya watoto wake 3 wa kwanza ‘‘kwa sababu ya UKIMWI,” anasema. ‘‘Nyembe zinapaswa kubadilishwa kila wakati lakini wakuu walikataa.”
Kwake, kama mmoja kati ya watu wa kabila la Otomari, alama hizo “hazina maana”. Utamaduni unawezwa kuendelezwa kwa njia nyingine, anasema, kupitia kwa lugha, densi, unyago na usanifu.
Watu wengi wa kabila la Otomari bado wanakubali kutiwa alama, wakiwemo wanawake kadhaa wachanga ambao wakati mwingine huchanjwa kwenye migongo yao na tumboni wanapobalekhe ili ‘‘kuonyesha ujasiri wako,” anasema Edith (aliyeonyeshwa kwenye picha). Mifumo huwa sawa mara kwa mara na michoro inayochorwa kwenye mijengo ya mitaani.
Wakati mwanawe Genevieve Boko, Marina (hapo chini) alipokuwa na umri wa miezi 6 tu alipotiwa alama – watoto katika sehemu zingine nchini Benin hufanyiwa kitendo hicho juma moja tu baada ya kuzaliwa.
Katika nchi jirani ya Nigeria, suala la haki za watu wachanga limesababisha baadhi ya majimbo kupiga marufuku zoezi hilo kwa watoto wote.
Hata hivyo, hii sio hatua inayowapendeza watu wote wa Benin. ‘Hatukiuki haki za watoto, tunawaonyesha watoto walikotoka na kile watakachopitia maishani,” anasema Telesphore Sekou Nassikou, mhariri mkuu wa kituo kimoja cha redio mjini Natitingou iliyoko kaskazini magharibi mwa taifa hilo.
Kwake, makovu hayo hupitisha ujumbe: ‘‘Tahadhari, kuna uchungu katika dunia hii, na utahisi uchungu katika maisha yako. Hata hivyo uchungu huo utaisha iwapo utavumilia.”

Nigeria:Maandamano dhidi ya serikali

Maandamano kuhusu wasichana waliotekwa
Maandamano makubwa ya kwanza yanatarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Nigeria- Abuja baadaye leo watu wakiitaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwanusuru wasichana 200 wa shule waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislam .
Wasichana hao walichukuliwa kutoka shule yao ya malazi iliyopo katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi kaskazini mashariki mwa nchi zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Waandalizi wa maandamano hayo wanaita serikali kuelekeza juhudi zao kwa wasichana waliopotea .
Mpango ni kuandamana hadi bungeni na kwa mshauri wa taifa wa masuala ya usalama na kuwasilisha barua ya kutoa wito wa kufanyika kwa juhudi zaidi kuwanusuru wasichana hao.
Mwanaharakati mmoja wa kijamii amesema katika nchi nyingine yoyote ile suala la kutekaji nyara wa wasichana hao wengi lingekuwa ni mjadala wa kila siku .
Lakini serikali ya Nigeria imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kukaa kimwa huku wazazi wenye shauku wakisailia kuwa gizani kuhusu nini kinachoendelea kuhusiana na wasichana wao.
Huenda kwa kuhisi hilo rais wa Seneti , David Mark, sasa amezungumza. Amewatolea wito watekaji kuawaachilia mara moja wasichana bila masharti na akasema bila shaka taifa letu liko vitani .

Watoto 9,000 walitumiwa vitani Sudan:K

Navi Pillay akiwa ziarani Sudan Kusini
Zaidi ya watoto 9,000 wamekuwa wakitumiwa kama wanajeshi katika vita vivayoendelea nchini Sudan Kusini.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa haki za binadamu katika umoja wa Mataifa Navi Pillay.
Pande zote kwenye mgogoro huu , wanajeshi na waasi wamedaiwa kuwasajili watoto kupigana.
Bi Pillay amesema kuwa Sudan Kusini inakabiliwa na tisho la njaa , lakini viongozi wake hawaonekani kuliona hilo kama swala muhimu la kushughulikiwa.
Alikuwa anazungumza mwishoni mwa ziara yake nchini Sudan Kusini ambako mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe umewaacha mamiioni ya watu bila makao.
Vita vilizuka mwezi Disemba kati ya wanajeshi wa serikali wanaomtii Rais Salva Kiir na hasimu wake kiongozi wa waasi, Riek Machar ambaye anatuhumiwa kwa kuanzisha mgogoro huu kwa kuwa na njama ya kumuondoa mamlakani.
Riek Machar pia wakati mmoja alikuwa makamu wa Rais wa Salva Kiir.
Machar amekanusha madai hayo lakini amekuwa akiongoza waasi wanaopigana dhidi ya serikali.
Pande zote mbili zimekuwa kwenye meza ya mazungumzo kujaribu kusitisha vita lakini hakuna mabadiliko katika hali inayokumba nchi hiyo, Vita vingali vinaendelea.

Uchaguzi Iraq

Uchaguzi kufanyika Iraq
Wapiga kura nchini Iraq wanashiriki katika zoezi la upigaji kura katika mikoa yote isipokuwa mkoa mmoja katika uchaguzi wa kwanza wa wabunge tangu wanajeshi wa Marekani waondoke nchini humo mwaka 2011.
Waziri mkuu wa sasa Nouri al-Maliki anagombea kiti chake kwa muhula wa tatu lakini kampeni zimekuwa zikipigwa kwa misingi ya vurugu za kisiasa zinazoendelea kukithiri nchini humo.
Selikali ya muungano ya bwana Maliki inayoongozwa na chama cha Kishia imekabiliwa na wakati mgumu kupambana na uasi unaongozwa na kundi lenye ufungamano na Al Qaeda katika mji wa Falluja na mkoa wa Anbar.
Sauti za mizinga zimekua taswira ya kila siku katika baadhi ya maeneo ya Iraq wakati kampeni za kuelekea uchaguzi huu.
Matokeo yake ni mashambulio ya kujitolea mhanga karibu kila siku.
Uchaguzi kufanyika Iraq
Helikopta za kijeshi zinashika doria katika anga ya Baghdad na serikali imefunga uwanja wa ndege na baadhi ya barabara kuu ndani na nje ya mji huo.
Hatua hizo zinanuia kuwapa imani wapigaji kura watakaojitokeza kwani ni bayana kuwa huenda vituo vya kupigia kura vikalengwa.
Watu 160 wameuawa wiki iliyopita huku wengine 275 wakijeruhiwa.
Baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa vikosi vya usalama vimepoteza maafisa elfu moja mwaka huu kwenye mapigano ya kukabiliana na uasi katika maeneo ya Fallujah na Anbar.
Inatabiriwa kuwa huenda Bw Maliki akashinda awamu ya tatu na kumuwezesha kuunda serikali ya muungano lakini ni bayana kuwa swala la usalama litasalia kuwa changamoto kubwa.

Idadi ya vifo Misri yazidi kuongezeka


Mwandishi wetu anasema aliona miili 140 ikiwa imefungwa kwenye sanda.
Wengi wa waathiriwa walifariki dunia katika mji mkuu wa Cairo lakini kulikuwa na vurugu katika maeneo yote ya nchi katika siku iliyoshuhudia umwagikaji mkubwa wa damu tangu mapinduzi ya kidemokrasia yaliyotokea miaka miwili iliyopita.

Keita ashinda uchaguzi wa urais Mali


Ibrahim Boubacar Keita ana jazi ngumu ya kukarabati nchi ya Mali
Ibrahim Boubacar Keita ameibuka mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Mali huku mpinzani wake akikubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais.
Soumaila Cisse,amekubali kushindwa na mpinzani wake,aliyekuwa waziri mkuu Ibrahim Boubakar Keita.

44 wauawa kinyama msikitini, Nigeria

Maiduguri ni moja ya majimbo yaliyowekewa sheria ya hali ya hatari
Takriban waumini 44 wameuawa kwa kupigwa risasi wakiwa msikitini Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa maafisa wa jimbo la Borno.
Mauaji hayo yalifanyika wakati wa maombi ya asubuhi Jumapili , ingawa taarifa zimejitokeza Jumatatu , kutokana na hitilafu ya mawasiliano kwani jimbo hilo liko chini ya sheria ya hali ya hatari.

WHEAT CLICK THIS PHOTO