Jaja
aliingia ‘mzima mzima’ pembezoni mwa lango la Thika kuhakikisha
anaiunganishia nyavuni krosi ya Msuva kwa vyovyote na akafanikiwa
akimuacha kipa Mganda, Hamza Muwonge anaokota mpira nyavuni.
Kwa
furaha ya bao hilo, Jaja ambaye alikuwa akizomewa na mashabiki wa Simba
SC kila alipokosea alitoka nje ya Uwanja kushangilia bao hilo, kwa
shangwe za aina zote alizoweza.
Yanga
SC haikucheza vizuri kipindi cha kwanza na zaidi ilitegemea kupitisha
mashambulizi yake pembeni walipokuwa wakiteleza kwa awamu Simon Msuva,
Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho.
Coutinho
alikaribia kufunga mara mbili kwa mipira ya adhabu aliyopiga kutoka nje
kidogo ya eneo la penalti, wakati Jaja hakuwa na madhara kabisa kipindi
cha kwanza.
Nafasi
nzuri zaidi kwa Thika ilikuwa dakika ya 20 wakati shuti la Moses
Odhiambo lilipodakwa na kipa Deo Munishi ‘Dida’- zaidi ya hapo, safu ya
ulinzi ya Yanga SC leo ilicheza vizuri.
Kipindi
cha pili, kocha Mbrazil Marcio Maximo alianza na mabadiliko katika safu
ya kiungo akimpumzisha Hassan Dilunga na kumuingiza Hamisi Thabit,
ambaye alikwenda kuibadilisha timu.

Simon Msuva
Mchezaji jaja kutoka kwenye timu ya yanga footbal club awa mchezaji nyota baada ya kuichapa timu ya rambramba Azam Fc bao mbili yeye mwenyewe uku baadae mchezeji Nyota wa Yanga Fc Simon Msuva kutundika bao la mwisho yani la tatu kwa wapinzani wao hao

mabovu story.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram , Twitter Na Facebook
No comments: