Hekaheka ya leo muigizaji maarufu Single Mtambalike maarufu kama
Richie, ameelezea hekaheka yake ya kusingiziwa Mtoto na mwanamke kutoka
Shinyanga ambaye alifika nyumbani kwake akiwa na mtoto mchanga na kudai
ni mtoto wa msanii huyo.
Richie amesema wakati huo ndoa yake ilikuwa changa na mke wake alikuwa na mtoto mchanga kitendo ambacho kiliitikisa ndoa yake.
Jamaa anasema hakuwahi kumwona mwanamke
huyo, hivyo baada ya kukasirishwa na kitendo hicho alijikuta akimpiga
mwanamke huyo makofi.
96.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tanga.
Hapa unaweza kuisikiliza Hekaheka yote kwa kubonyeza play.
No comments: