Nyota
wa muziki kutoka nchini Marekani Katy Perry ameshtakiwa na marapa nyota
wa nyimbo za Injili akiwemo mwanamuziki Flame ambaye amedai kuwa nyimbo
ya Dark Horse ya Katy imeiba baadhi ya mistari kutoka kwenye nyimbo yao
ya Joyful Noise.
Wanamtuhumu Katy Perry kwa kutumia nyimbo yao iliyotoka mwaka 2008
waliyomshirikisha Lecrae bila ruhusa na kuharibu ujumbe wa kidini uliopo
ndani ya nyimbo hiyo na kutumia picha za “kichawi” na nguvu za kidunia.
Nyimbo ya Dark Horse iliongoza katika chati za muziki za Billboard kwa wiki kadhaa mwezi January.
Kundi la marapa wa nyimbo za injili Flame aka Marcus Gray, Lecrae
Moore, Emanuel Lambert na Chike Ojukwu wanataka kulipwa fidia na
mwanamuziki huyo,, studio yake ya Capitol, na waandishi wa nyimbo Dr
Luke na Max Martin kwa kuiba hakimiliki za wimbo wao.
Hii ndio sababu ya Katy Perry kushtakiwa na marapa wa nyimbo za Injili.

No comments: