Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel
Sitta amekiri “kuchezewa” kwa saini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere na sehemu ya saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la
Tanganyika, Pius Msekwa zilizopo kwenye hati ya sheria ya kuridhia
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta
alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya
1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa.
Alisema katika saini ya Nyerere
kumeongezwa herufi “us” kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa
kumeandikwa neno “Msekwa” kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta
alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo
hayasomeki, lakini walifanya makosa.
“Wale vijana walipoona document
(nyaraka) haisomeki waliongeza “us” mwisho kwa kompyuta kwenye saini ya
Nyerere, ila walifanya makosa maana bora kitu kionekane kufifia hivyo
hivyo lakini kibaki na maana yake,” alisema.
Hata hivyo, Sitta alisema kwa waliofanya
kazi na hayati Baba wa Taifa wanatambua saini iliyopo kwenye hati ya
sheria hiyo ipo sawa ukiondoa makosa ya kuwekwa herufi hizo.
Kuhusu saini ya Msekwa, alisema pia kulifanyika makosa katika sehemu ya saini hiyo, kuandikwa kwa kompyuta “Msekwa”.
“Ni saini ya Msekwa, lakini vijana wa
chamber kwa AG waliongeza neno “Msekwa” kwa kompyuta. Ni mtu asiyejua
thamani na uhalisia wa saini ni kubaki ilivyo hata kama kwa miaka 100
hata mtu aje kuisoma kwa darubini,” alisema.
Hata hivyo, alisema maudhui ya hati ya
sheria hiyo, iliyosainiwa rasmi Aprili 25, 1964 ni sahihi kama ambavyo
walikubaliana waasisi wa Muungano, Nyerere na Karume.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alisema kwamba
hafahamu kama ofisi yake inahusika na kuchezewa kwa saini hizo, tofauti
na madai ya Sitta.
Sheria iliyopitishwa Z’bar
Sitta alisema ili kuondoa utata,
ameagiza kupatiwa hati ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume
(Presidential Decree) aliyotoa kusaini makubaliano kwani wakati huo,
hakukuwa na Bunge.
“Karume alitumia Baraza la Mapinduzi
akatumia amri ya Rais akasaini. Tunatarajia kuipata hiyo, sasa tutakuwa
tumepata nyaraka za Bara na Zanzibar,” alisema Sitta.
Latest
m.media photographer_mimi. Powered by Blogger.
Featured author
admin
PostsThe Admin is a powerful person in this world, more powerful than the president of USA. The very mention of admin sends shivers down the president. You have been warned!
Tagged with: HABARI.COM
About ujugu
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ABOUT ME
- Popular Post
- Video
- Category
HOT NEWS
-
Diamond akiwa na mkubwa wake wa kazi
-
Since its founding, Ketebul has been focused on ‘Bridge’ artists – the key artists that created certain genre that link the tribal mus...
-
Wanajeshi wa Brigedi Maalum wakiwa katika mazoezi makali yaliyofanyika hivi karibuni huko Goma Mashariki ya Demok...
No comments: