Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amewataka wasanii wenzake wa Tanzania kumuunga mkono Diamond na AY baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye kampeni ya kilimo inayohamasisha vijana wa Afrika kukipa nafasi kilimo.
Akizungumza kwenye kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio hivi karibuni,Ben Pol alisema hakuna haja wa kuwa mtimanyongo kwa Diamond na AY.
“Mimi nachoweza kusema ni kwamba hao ni ndugu zetu,wameenda kutuwakilisha vizuri,yaani hakuna haja ya kuwa na mtima nyongo,yaani ‘ooh ‘dah kwanini sio mimi’ hapana! Kwasababu hiyo imekuwa hivyo kwasababu wametakiwa watu wawili, kwahiyo suala ni watu wawili wowote wanaweza wakaenda kurepresent, ni suala jema ndo tunavuka mipaka, itasaidia mabadiliko mengi ikiwa pamoja na masuala ya bei na value ya msanii.Kwahiyo tunapata exposure tunajaribu kujifunza pia vitu vingi itatusaidia as wasanii,” alisema.
No comments: