Mkasi ni kipindi cha TV kilichoanzishwa na msanii na mfanyabiashara Ambwene Yessaya aka AY, kipindi kilichojipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania.
AY yuko nchini Kenya ambako pamoja na mambo mengine ameenda kuzindua video yake mpya ya ‘Asante’ iliyotoka weekend iliyopita.
Kwa mujibu wa Nairobi Wire, AY ameenda Kenya na crew ya Mkasi ambao ni Salama Jabir na Josh Murunga, kwa ajili ya kuangalia fursa zinazoweza kupatikana nchini humo kwa lengo la kutaka kupanua wigo wa kipindi hicho.
“Tuko hapa kwanza kuangalia uwezekano wa kupanua biashara ya kipindi chetu” Alisema AY.
Wiki iliyopita msimu wa mkasi ulimalizika kwa Salama kumhoJi AY, na moja ya vitu alivyovisema AY kuhusu kipindi ni pamoja na hiki:
“Season inayokuja itakuwa ni revolution kama ambavyo tumefanya mwanzo…kwa kweli ni kuwa watu ambao wana akili zao watu ambao wana lengo moja kwa pamoja ni timu ambayo inafanya kitu pamoja na tunafanya kitu kimoja ambacho kinawafundisha na watu wengine”.
Msimu mpya wa Mkasi ambayo hurushwa kupitia EATV unatarajiwa kuanza Julai Mosi.
-Bongo5
No comments: