Nick Dizzo ameiambia Bongo5 exclusively kuwa kwa sasa ana kampuni yake mpya iitwayo ‘Focus Films’ ambayo imechukua nafasi ya E-Media aliyokuwa akishirikiana na Sama Jahn.
“E-Media pia ilikuwa company yangu, ila kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu kwa sasa natumia company yangu mpya ya Focus Films, ina team mpya ambayo iko focused zaidi kwenye kazi”.
Dizzo ambaye pia alidirect video ya Quick Rocka ‘My Baby’, amesema kampuni ya E-media haitakuwepo tena, pia kuanzia sasa atakuwa akisimama mwenyewe kama director tofauti na mwanzo kila video ilikua inasomeka majina mawili likiwemo la Sama Jahn.
“one of the changes pia ni hivyo, nitakuwa niko peke yangu kama director”.Alisema Dizzo
Baadhi ya video zingine zilizotayarishwa na Nick Dizzo chini ya E-Media ni pamoja na ‘Love Me’ ya Izzo B, ‘Nafanya’ ya Cyril ft. Jux, ‘Going Crazy’ ya Hemed PHD na ‘Lovely’ ya Gelly wa Rhymes.
Tummoghele ya Izzo B na Nishike mkono ya D-Knob ndio za kwanza kufanywa na Nick Dizzo kupitia Focus Films.
No comments: