Marehemu Ahemed mgeni enzi za uhai wake |
Mwimbaji huyo mashuhuri aliyewahi
kutamba kipindi cha nyuma na bendi za Zanzibar Stars na Baadae New
Zanzibar Stars na mpaka mauti yanamkuta alikuwa katika bendi ya Zanzibar
Njema ambayo alikuwa anaiimbia mpaka sasa.
Mwimbaji huyo alikuwa
anasumbuliwa na maradhi hayo toka akiwa Dubai baada ya hapo alirudi hapa
nchini na kufikia Unguja nyumbani kwao na kulazwa katika hospital Mnazi
mmoja Kisiwani humo aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupata nafuu
lakini alirudishwa tena hospital baada ya hali yake kuwa mbaya mpaka
mauti yamemkuta alfajiri ya leo akiwa hospital.
Taarifa kutoka kwa familia ya
marehemu zinasema mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni huko huko
Unguja,Zanzibar. Mpaka mauti yanamfika marehemu Ahmedi Mgeni alikuwa
bado hajaaliwa kuwa na mwenza wa maisha yake (hajaoa)
Ahmed Mgeni mpaka mauti yanamfika hii leo alikuwa ni Kiongozi wa bendi hiyo ya Zanzibar Njema Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi amina,Tunaungana na familia yake pamoja na wapenzi muziki wa taarab nchini kwa kumpoteza mwimbaji huyo mashuhuri wa muziki wa taarab.

Moja ya nyimbo ambazo marehemu amefanya wakati wa uhai wake na ilitamba sana ni wimbo wa Sitetereki.
No comments: