Kwenye mahojiano zaidi ya ‘Sema Yote’
aka Tell it All exclusive kwa Bongo5, Ommy Dimpoz amemzungumzia mchumba
wake na jinsi ambavyo anapenda kuwa na watoto wa kike kuliko wa kiume.
“Nina mchumba, watu wengi hawajui kuhusu
mahusiano yangu lakini nina mchumba na natarajia Mungu akijalia ntakuja
kumuoa. Yupo nje bado anasoma. Akimaliza shule ntamuoa,” alifunguka
Ommy ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara ya wiki tatu.
Swali ni Je! Mchumba huyo ni nani? Leo
kupitia Instagram, ameshare picha ya msichana mrembo aitwaye Emmy na
kusababisha maswali mengi kama ndiye yeye au lah.
Emmy
“My Biggest fan in Swiss Emmy Mwarabu,” aliandika.
Katika hatua nyingine Ommy Dimpoz
alisema anapenda kuja kuwa na familia ya watoto wasiozidi watatu na
anapenda watoto wa kike zaidi.
“Lakini mimi napenda watoto wa kike
zaidi. Basi tu automatically nimekuwa hivyo. Pengine ni kwasababu
nimelelewa sana na mama yangu.”
Hata hivyo alisema hatopenda kuona wanae wanakuwa wanamuziki kama yeye.
“Kwa maisha ya muziki ninavyoyaona na jinsi ilivyo hii kazi nisingependa mwanangu afanye,” alisema.
No comments: