MAUAJI ya watu watatu wa familia moja
yaliyotokea jijini Mwanza hivi karibuni yameibua maswali mengi lakini
mwisho wa yote, imebainika kuwa kilichoiponza familia hiyo kukumbwa na
mauti hayo ni hiki, Uwazi limechimba mwanzo mwisho.
Mauaji hayo yalitokea saa 10 alfajiri ya
Septemba 21, mwaka huu katika Kijiji cha Ihila, Kata ya Buhongwa,
Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza ambapo inaaminika kuwa mgeni
aliyekaribishwa kwenye familia hiyo ndiye aliyetekeleza mauaji hayo na
alikaribishwa nyumbani hapo bila kujulikana tabia.
Debora Jonas Luhinga, mtoto wa marehemu
ambaye alinusurika katika tukio hilo, alisema kuwa mgeni huyo
aliyemfahamu kwa jina moja la Lameck alifika nyumbani hapo Septemba 18,
mwaka huu lakini baada ya kutekeleza mauaji hayo alitokomea
kusikojulikana.
Debora mwenye umri wa miaka 12, alidai
kuwa siku ya tukio, usiku akiwa amelala, mdogo wake aitwaye Eliudi
aliyekuwa amelala naye aliamka na kuanza kulia sana.
Alisema alichukua jukumu la
kumbembeleza mdogo wake huyo lakini ilishindikana, ghafla Lameck
aliingia chumbani humo na kumwomba mtoto huyo ili ampeleke chumbani kwa
wazazi wake akabembelezwe.
“Kilio cha mdogo wangu kilikuwa kikubwa,
mara nikaona mlango unafunguliwa, Lameck akaingia, akasema kwa kuwa
mtoto analia sana nimpe ampeleke kwa mama ili akambembeleze,” alisema
Debora.
Akaongeza kuwa alikubali kumpa Lameck mtoto huyo na kwa vile yeye alikuwa na usingizi mzito aliendelea kulala fofofo.
Debora alisema alipoamka kulikuwa kumekucha, akashuka kitandani ili aende nje lakini akakuta mlango umefungwa kwa nje.
“Nilipiga kelele baada ya kukuta mlango
wa chumba changu umefungwa kwa nje, majirani walifika kunifungulia
lakini nilipigwa na mshangao kukuta maiti ya baba ikiwa sakafuni
sebuleni tena imetapakaa damu.
“Nikiwa nimechanganyikiwa niliingia
chumbani kwa wazazi wangu, nikashangaa kumuona mama yangu na mdogo wangu
Eliudi wakiwa wameuawa kwa kunyongwa na miili yao imelazwa chini,”
alisema Debora.
Debora alisema anaamini Lameck ambaye
mara nyingi alikuwa akimwona akizungumza na baba yake ndiye aliyetenda
unyama huo. Alisema anaamini mtu huyo wakati anaingia chumbani kwake
kumchukua mdogo wake alikuwa ameshawaua wazazi wake na aliamua kumtwaa
mtoto huyo kwenda kumnyonga ili kilio chake kisiwafanye majirani
wakafika nyumbani hapo kutaka kujua kulikoni na hivyo kugundulika
alichokifanya kwa muda huo.
Alikwenda mbele zaidi kwa kusema anaamini baba yake ndiye aliyeanza kuchinjwa kabla ya mama yake kunyongwa.
Baadhi ya majirani waliozungumza na
gazeti hili huku wakiomba majina yao kuhifadhiwa baada ya tukio hilo,
walisema kwa nyakati tofauti kuwa huenda mauaji hayo ni ya kulipiza
kisasi kwa mwanaume huyo ila mkewe na mtoto waliingizwa kwenye mkumbo
tu.
Walisema haiwezekani watu wa familia moja wakauawa kikatili namna hiyo bila ya wauaji kuanika sababu.
Waliongeza kwa kudai kuwa siku zote tatu alizoishi hapo, Lameck alikuwa akitafuta njia mwafaka ya kutekeleza ukatili huo.
Walisema mauaji mengi ya aina hiyo
yanayotokea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza huhusishwa na
imani za kishirikina, migogoro ya ardhi au mirathi.
Majirani hao waliongeza kuwa awali
walikuwa wakimwona Lameck nyumbani kwa marehemu bila kujua uhusiano wao,
wakaonya kuwa ni hatari sana kumkaribisha nyumbani mtu usiyemjua kwa
undani kama ilivyokuwa kwa Lameck.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP
Ernest Mangu alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku akisema hakuna
aliyekamatwa. Aliwataja marehemu kuwa ni Jonas Luhinga, mkewe Rusia
Jonas na mtoto wao, Eliud Jonas.
Latest
m.media photographer_mimi. Powered by Blogger.
Featured author
admin
PostsThe Admin is a powerful person in this world, more powerful than the president of USA. The very mention of admin sends shivers down the president. You have been warned!
Home
Matukio
MGENI ACHINJA BABA NA MAMA WA FAMILIA NA KUMNYONGA MTOTO WA MIEZI 7 HUKO JIJINI MWANZA.
Tagged with: Matukio
About ujugu
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ABOUT ME
- Popular Post
- Video
- Category
HOT NEWS
-
Diamond akiwa na mkubwa wake wa kazi
-
Since its founding, Ketebul has been focused on ‘Bridge’ artists – the key artists that created certain genre that link the tribal mus...
-
Wanajeshi wa Brigedi Maalum wakiwa katika mazoezi makali yaliyofanyika hivi karibuni huko Goma Mashariki ya Demok...
No comments: