Mwanamke huyo raia wa Ufaransa aliyejitambulisha kwa jina moja la Pauline amesema alifanikiwa kujiokoa kutoka katika mall ya Westgate akiwa na watoto wake wawili wadogo ambao walipewa Chocolate na magaidi hao.
Habari hiyo inaendelea kusema mama huyo wa watoto wawili, ambaye alikuwa katika mall ya Westgate wakati mashambulizi hayo yanaanza, alisema baada ya kuwaambia magaidi hao kuwa ‘Waislamu sio watu wabaya’, magaidi waliwapatia Chocolate watoto wake wawili Emily (6), na Eliot (4).
Pauline amedai kuwa aliombwa msamamaha na magaidi hao waliomwambia kuwa wao sio monsters “we are not monsters”.
Aliongeza kuwa magaidi hao wenye silaha walimwambia kuwa wanahitaji kuwauwa wakenya na wamarekani pekee na wakamwambia abadilishe dini awe Muislam kisha wakamuomba msamaha mwanamke huyo “do you forgive us? do you forgive us?’.
Mwanamke huyo amesema alifanikiwa kujiokoa na watoto wengine wawili, akiwemo mvulana wa miaka 12 ambaye mama yake aliuwawa katika mashambulizi hayo.
No comments: