KATIKA hali ambayo ni ya kushangaza, mkazi wa Kata ya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kukutwa akifanya ngono na mbwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alitaja jina la mtu huyo (jina tunalihifadhi), akisema anadaiwa kukutwa akifanya kitendo hicho usiku wa kuamkia jana kwenye chumba chake.
Kamanda Boaz alisema majirani zake, ndiyo walishuhudia na kutoa taarifa polisi. Mtuhumiwa anadaiwa kukimbia kusikojulikana.
Mbwa huyo anamilikiwa na mtoto wa mtuhumiwa. Kwa mujibu wa kamanda, mtuhumiwa ana familia ya wake watatu.
Polisi inamtafuta mbwa husika kumfanyia uchunguzi.
Akizungumza nasi , Daktari wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC, alisema mtu anayefanya kitendo hicho na mnyama, anahitajika kufanyiwa vipimo, kubaini kama yuko sawa.
"Kwa kawaida sio jambo la kawaida, anaweza kuathirika kisaikolojia na jamii kumchukulia mtu wa tofauti kama amelaaniwa au ni kichaa, pengine anahitajika kufanyiwa vipimo kuonekana kama yupo sawa," alisema.
No comments: