Muimbaji wa kike wa Nigeria, Adokiye Kyrian amesema bado ni bikira na ataendelea kuwa hivyo hadi pale atakapopata mwanaume sahihi.
Kwenye mahojiano na jarida la Vanguard, muimbaji huyo mrembo alisema: Hujawahi kuona msichana mrembo ambaye ni bikira? Mtu yeyote atakayemnunulia mama yangu ndege binafsi nimemuahidi (mama yangu) ataushika moyo wangu.”
Aliongeza kuwa haamini katika mapenzi na ana uhusiano na career yake tu. Amesema usanifu wa majengo (Architecture) ndiye mumewe muziki ndio boyfriend wake. Adokiye anaamini kuwa mapenzi ni hatari na kwamba hakuna mapenzi ya kweli. Akiwa na miaka 23 muimbaji huyo sasa ni balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa.
No comments: