Shirika la ndege la Malaysia
limewaambia jamaa na familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege
iliyotoweka MH370 kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura.
Tangazo hilo limetolewa kwa familia hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.Aidha tangazo hilo limekuja huku juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara Hindi zikimalizika kwa siku ya tano bila mafaniko.
Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.
Aliambia waandishi wa bahari kuwa udadisi uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth mbali na eneo lolote la kutua.
Ameomba vyombo vya habari kuheshimu familia za watu waliokuwa ndani ya ndenge hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa taarifa mbaya hata zaidi.
Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza mawasiliano wiki mbili zilizopita na meli za nchi mbali mbali pamoja na ndege zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata chochote.
story habari by www.bbcswahili.com
No comments: