Utamaduni wetu Tanzania na kama ilivyo kwa mafundisho ya dini kupitia
vitabu vinne vitakatifu, Torati, Zaburi, Injili na Kuran, fundisho ni
kwamba mja aliyepoteza maisha hakashifiwi, hasimangwi, hahukumiwi,
isipokuwa huhifadhiwa kwa heshima kisha kuombewa salama na amani mbele
ya Mungu.
Ommy Dimpoz, kijana ambaye ni mwaka jana tu alikuwa ‘anawanga’ huku na huko mikono nyuma akiomba msaada wa kimuziki, hivi sasa anajiona ameota meno ya juu kuweza kung’ata, kiburi hicho kimempa uthubutu wa kumtusi Mfalme wa Freestyle, marehemu Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwair’.
Thamani ya Ngwair na namna alivyozikwa kwa heshima hajaviona, badala yake akatusi kuwa Mfalme wa Freestyle alikufa maskini ndiyo maana mazishi yake yalikuwa ya kuungaunga michango ya wadau.

Kifo cha Ngwair, kilivuta makundi mbalimbali kushiriki kwa hali na mali kuchangia na kumzika, taifa lilizizima mkoa kwa mkoa, mguso huo wa kitaifa aliokuwa nao mwanamuziki huyo, Ommy hakuuona, isipokuwa akanena: “Sitaki kufa maskini kama Ngwair.”maneno hayo aliyatoa ommy dimpozi alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa mpekuzi leo hii habari na picha mpekuzi posted by MABOVU STORY
No comments: