Slider[Style1]

HABARI

BONGO MOVIES

BONGO FLEVA

.

BONGO VIDEOS

Style5[ImagesOnly]

STORY ZA INSTAGRAM

                              Tuliendelea kwa miezi kadha na huyu kijana huku na mimi nikiwa na bosi wangu
 kule kazini , basi bwana siku moja , sisi officini tulitakiwa kwenda kutoa damu hospitali ya muhimbili katika maadhimisho ya siku ya afya duniani . Watu walipimwa afya zao na mimi nilipimwa , majibu yangu yalikuwa ya kutatanisha sikuamini macho yangu wala masikio yangu , nilienda hospitali ingine napo majibu yalikuwa yale yale kwamba nimeadhirika na UKIMWI .
haya sasa hapo ndipo tulipo ishia wiki ya jana sasa waweza soma tena mwendelezo wa simulizi hii ya NAJUTA KUTEMBEA NA BOSI!


Haya majibu yalimfikia mpaka bosi wangu nae akatambua hilo akasikitika sana nay eye alivyoenda kupimwa akakutwa hajaadhirika , basi nikajua moja kwa moja ukimwi nimepata kutoka kwa yule kijana wa mitaani na sio mtu mwingine .
Nikamwomba huyu kijana tukaangalie afya zetu kwa mara ingine tena hospitali , tukaenda kule kupima afya zetu , yeye ndio alikuwa wa kwanza kupokea majibu yake , alikutwa ameadhirika akupata mshituko wa ghafla yaani haamini .
Mshituko huo ulimpelekea aanguke chini na kuzimia watu walienda kumbeba na kumpeleka hospitali kupatiwa huduma ya kwanza basi hapo ndio magonjwa mengine yalianza kujitokeza na kujulikana sana .
Kumbe huyu kijana alikuwa na urafiki wa kimapenzi na shugamami mmoja mtaa wa pili huyu shuga mami mume wake alifariki dunia miaka 5 iliyopita kwa UKIMWI watu wanaema TB sijui , ndio huyu kijana kuona zile pesa za shuga mamy akaenda kwake .
Kijana aliumwa kwa miezi 3 hivi kisha akafariki dunia akaniacha duniani mwenyewe , kule kazini nilifukuzwa kaza na bosi wangu kisa nilitaka kumwambukiza ugonjwa wa ukimwi , lakini siku moja alinipigia simu kunieleza kwamba mke wake ameadhirika na UKIMWI pia lakini yeye anasema hajaadhirika .
Hapo ndio nilishangaa sana , kwanini mke wa aadhirike yeye asiadhirike au mke wake nae alikuwa anatoka nje ya ndoa bila mume wake kujua ? basi hiyo ni siri yao nyumbani kwao mimi hayanihusu .
Lakini ndio hivyo nilikuwa nimeshaadhirika na UKIMWI kazi nimeshafukuzwa sina cha kufanya wala kutafakari nilifikiria zaidi kuhusu ugonjwa wangu wa UKIMWI na jinsi nitakavyoweza kuishi maisha marefu kwa matumaini .
KAHABA
Baada ya kuona maisha magumu na sina lolote la kufanya mimi kama mwanamke mrembo na mwenye mvuto niliamua kutafuta njia rahisi zaidi ya kujipatia kipitano nilifikiria njia nyingi sana ambazo zingeweza kunipatia angalau mlo na mavazi katika siku zangu za maisha zilizobakia baada ya kugundulika nina virusi vya ukimwi
Nikaanza kutafuta sehemu ambazo naweza kuuza mwili wangu kwa pesa za chapchap niweze kuendeleza maisha yangu ya kila siku , nilikuwa na ramani yangu kwanza pale OHIO , JOLLY , MACHENI , BILLS NA LATAVERNA hizo ni sehemu 5 kuu za starehe jijini dare s salaam kwahiyo huko naweza kufanya kazi za kujiuza kwa wiki nzima kila siku bila kuchoka .
Ohio ilikuwa nzuri ila tatizo lake ni kwamba kila anayepita pale anakujua halafu unatakiwa uonyeshe maungo yako hazarani mimi sikuzoea tabia hizo na sikuwa na mhemko huo kwahiyo nilivaa miwani yangu na kuacha mapaja nje tu waangalie wenyewe kama wanapenda watakuja . Kule macheni tatizo lake ni mashoga wengi sana , yaani mwanaume anaweza akaja kutafuta Malaya akakuchanganya wewe ni shoga , wale mashoga wanaojiuza hawana tofauti na sisi wanawake tunaojiuza wakati Fulani ulitokea ugomvi mkubwa watu waliamulia tulimgombea mwanaume .
Billa nako kuzuri ila vijana wengi sana halafu hawana pesa , na vitoto vidogo vingi , nilikuwa naogopa matatizo na vijana wa kule sikupenda kufanya mchezo na watoto wadogo waliokuwa wananitaka hata kwa dau gani nilingoja wanaume wenye pesa zao tu sio zaidi .
Basi nilianza safari za kuelekea jolly club kwa ajili ya kujiuza mwili wangu nipate angalau chochote cha kula na kufanya katika maisha yangu , pale jolly club nilikutana na dada mmoja anaitwa Aisha , huyu dada nae ni kahaba mzoefu akaanza kunionyesha mambo kadhaa wa kadha kuhusu biashara ya ukahaba na kadhalika . Hapa ndio nilijufunza kwamba sio makahaba wote ni masikini au hawajiwezi kuna wengine wanajiweza na wanazo fedha ila wanapenda kufanya ukahaba yaani wamechoka na dunia wengine walikuwa na wanaume wao wakaachika wakaamua kuja huku kwenda na mwanaume wowote yule anayekuja .
Wengine wana matatizo katika ndoa zao kupigwa na kadhalika wanaamua kuja huku kujiuza au kukaa huku ili kuepuka matatizo katika ndoa zao au mahusiano yao , wengine ndio kama hivyo waume zao hawana nguvu za kutosha kufanya nao tendo la ndoa wanaamua kuwa makahaba kila mtu na lake na mambo yake pia .

About ujugu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

WHEAT CLICK THIS PHOTO