
Nilikua mwajiriwa katika kampuni moja maarufu jijini
dare s salaam , katika kuajiriwa kwangu huko nikawa msaidizi maalumu wa
bosi wa kampuni ile , basi siku moja moja nilikuwa naenda kujirusha na
bosi wangu .
Ukizingatia kwamba sikuwa na mume wala mchumba na
kwa kweli huyu bosi ndio alikuwa mtu wa kwanza kufanya nae tendo la ndoa
, hivyo nilifurahia mhemko wake na jinsi alivyokuwa ananipenda na
kunijali kila kitu nilipata na zaidi .
Alifanya yote haya bila kunificha kwamba ana mke na
watoto nyumbani kwake kwahiyo wakati mwingine chochote kinaweza kutokea
nijiandae kwa shuguli hiyo pevu kama mke wake akishitukia dili hilo .
Tulikuwa na uhusiano na huyu bosi kwa miezi 4 hivi
mpaka siku moja katika tembea tembea mitaani nikakutana na kijana mmoja
mtanashati akanieleza kwamba ananipenda na kunizimia sana yaani
ameshanifia
Huyu kijana alihangaika kwa mwezi mzima mpaka siku
nikaja kumkubalia akawa ndio mpenzii wangu halali sasa , nilimwamini
sana nay eye aliniamini sana , miezi 3 tokea kujuana na huyu kijana
aliniambia kuhusu kufanya nae tendo la ndoa .
Nilifikiria sana wakati mwingine nilitaka kulia
jinsi alivyokuwa ananishika na kuniomba tendo la ndoa akiwa chumbani
kwangu , alijaribu kunishika sehemu kadhaa akanivua nguo nami nilimtolea
nje nilimkatalia .
Basi siku moja nikamwomba tukaangalie afya zetu ,
kijana wa watu alikasirika sana wiki nzima hakufika nyumbani kwangu wala
kunipigia simu , kumbe alitaka tufanye tendo la ndoa bila kinga ? sasa
ningejuaje kuhusu afya yake ? au ananiamini nini mimi ?
Maisha yaliendelea na mambo mengine yaliendelea tu
wiki ya 3 alinipigia simu akaniomba msamaha turudiane na alikubali
kwenda na mimi kupata vipimo vya afya zetu kujua kwanza kabla hatujaanza
mambo mengine yoyote yale .
Basi ndio hivyo majibu yaliyoka mazuri , ndio
mapenzi yetu alikuwa zaidi na penzi nilimpa bila hiyana wala aibu yoyote
, yeye mwenyewe alifurahia mambo yangu na kwanza alikuwa anatoroka
nyumbani kwao kuja kulala kwangu wakati mwingine mwezi mzima .
Tuliendelea kwa miezi kadha na huyu kijana huku na
mimi nikiwa na bosi wangu kule kazini , basi bwana siku moja , sisi
officini tulitakiwa kwenda kutoa damu hospitali ya muhimbili katika
maadhimisho ya siku ya afya duniani . Watu walipimwa afya zao na mimi
nilipimwa , majibu yangu yalikuwa ya kutatanisha sikuamini macho yangu
wala masikio yangu , nilienda hospitali ingine napo majibu yalikuwa yale
yale kwamba nimeadhirika na UKIMWI . USIKOSE KUFATILA MAKALA HAYA JUMA PILI IJAYO kumbuka makala haya yameletwa kwenue na youth africa company
No comments: