Muigizaji wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi) amefariki dunia leo
mchana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kashi amewahi kutamba na mchezo wa ITV, Tamu Chungu akiwa na wasanii wenzake kama Mzee Masinde,Samson na wengine.
Baada ya kupata habari hii, mwandishi wetu aliongea na muigizaji mwenzake
Monalisa ambae amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Monalisa amesema
alipata taarifa jana kwamba Kashi amelazwa hospitali akiwa amezidiwa
kiasi cha kushindwa kuongea na hivyo kushindwa kujua nini kilikuwa
kinamsumbua.
Naye Hemedy PHD ametweet: REST IN PEACE MUIGIZAJI MWENZETU JAJI
KHAMIS KASHI….MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI…MOVIE YA MWISHO TULICHEZA WOTE
ILIKUA MATILDA!!Sad newz
No comments: