Amina Mwamkinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na
wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo wakimtuhumu kuwa mchawi
majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi
aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na
baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Hapa Amina akimsimulia mkasa mzima mwandishi wa Mbeya yetu Joseph
Mwaisango mara baada ya kupata maelezo yote ya Amina mwandishi wetu
alimpigia simu katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mbeya afike ofisi ya
Mbeya yetu ili wasaidiane kutatua tatizo hilo
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alifika ofisi ya Mbeya yetu na kuanza kumsikiliza Amina.
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale akiwa makini kumsikiliza Amina katika ofisi ya Mbeya yetu
KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood
iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule
Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa
anajihusisha na imani za Kishirikina.
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni
mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo
tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa
kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa
tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa
jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura
mitaani asijue hatma ya maisha yake.
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa
alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo
majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi
aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na
baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo
haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo
baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu
yake.
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun iliyoko Jijini
Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata
huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na
masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa
simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba
walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa
wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili
ahamie.
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alisema
alikuwa halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti
angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule
umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa
kwenye shirika linalolipa.
Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume
amesema kwamba hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo na kuongeza
kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya
kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka
ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida.
No comments: