Slider[Style1]

HABARI

BONGO MOVIES

BONGO FLEVA

.

BONGO VIDEOS

Style5[ImagesOnly]

STORY ZA INSTAGRAM

Baada ya kuambiwa anaujauzito, Hii ndiyo picha aliyo post Aunt Ezekiel na kuandika haya


Baada ya wengi kuongea na baadhi ya vyombo vya habari zikiwemo na blogs kuandika kuwa Aunt Ezekiel anaujauzito na hadi kufikia kudhaniwa ni nje ya ndoa pamoja na mmoja wa wanenguaji wa msanii Diamond Platnumz kuhisiwa anahusika, Masaa 24 yaliyo pita kupitia account yake ya instagram Aunt Ezekiel ameandika haya.
Lazima ujue Kutofautisha kati ya Kitambi na Mimba Sasa hiki Chagueni wenyewe ni KITAMBI AU MIMBA!!!!!legoooooooooo......

Hemedy Kuja Na Video Mpya Jina Na Lini Inatoka Viko Hapa. #TwitZaMastaa

Kama ilivyo kawaida kwa Hemedy Phd kutoa kazi na video mapema ili mashabiki wapate vyote kwenye radio na tv, Hii itatokea kwenye wimbo wake mpya GoodMorning. Video inatarajiwa kutoka December
 
 

Soma alichoandika Masanja Mkandamizaji kuhusu uhusiano wa Wema na Diamond

WEMA
Masanja mkandamizaji mchekeshaji kutoka kundi la Komedi Orijino kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika mawazo yake juu ya uhusiano wa Wema Sepetu na Diamond.
Hiki ndicho alichoandika,”Hili swala la diamond na wema nadhani mungu amemuhurumia mmoja wapo kati ya hao wawili. Kama wangekuwa watu wa kuoana wangesha oana uchumba gani mrefu kama wanasomea udokta????
Rafiki yangu nasib, kama kweli mlipendana kwa dhati hizo kasoro zinarekebishika, maana hakuna mwanadamu aliye sahihi kwan hata ww nasib unamapungufu yako. Na wewe dada yangu wema lazima ujue mme ndio kichwa cha nyumba kwa maelezo hayo inaonyesha haumsikilizagi mwenzio omba msamaha tenaaa na tena na ukubali kubadilika.
Mi sipendi mkiwa mnaongozana wote kwenye ma show ya usiku mme kafanye kazi mke abaki home ukirudi mwili umepoa hata ujauzito unaingiaa!! Sasa woote stejini mkirudi miili ya moto si mtazaa popompoo jamaniii!! Nitafurahi kusikia tofauti zenu mmezimaliza kwa amani ili mashabiki wenu wasijisikie vibaya
WEMA2

Inasemekana Hii Ndio Couple Mpya Ya Mastaa Duniani.

Jennifer Lawrence Na Chris Martin
Jennifer Lawrence Na Chris Martin
Mpenzi wa habari za burudani duniani utakuwa umegundua trend inayoendelea kwa sasa ya couple nyingi za masta kuvunjika kwa sababu tofauti, Stori mpya ambayo imeenda tofauti ni kuhusu tetesi zilizosamba kuwa mwigizaji Jennifer Lawrence na kiongozi mwimbaji wa bendi ya rock ya Cold Play Chris Martin ni wapenzi.
Vyanzo vingi vimeripoti kuwa tayari mashabiki wa watu hawa maarufu wamejumuisha majina yao na kuanza kuwaita “Martin Lawrence” . Ndoa ya Chris Martin ambaye ni rafiki wa karibu wa familia ya The Carters [Jay z Na Beyonce] ilivunjika miezi michache nyuma.

Star mwingine kutoka Tanzania ambaye page ya Facebook imekuwa verified

hasheeeeeemAlama ya verified ndio inatambulisha ukurasa halali wa mtumiaji kwenye mitandao mingi sana. Alama hii ni muhimu sana hasa kwa watu maarufu wanaotumia mitandao ili kuepuka kuwepo kwa kurasa feki ambazo haziwahusu.
Hivi sasa mtu maarufu ambaye page yake ya facebook imekuwa verified ni mchezaji wa kikapu kwenye timu ya Oklahoma City Thunders “Hasheem Thabeet”. Ukurasa wake wa twitter ulikuwa verified siku nyingi na hivi sasa mashabiki wake wa facebook watakuwa na uhakika kwasababu na facebook wame-verify ukurasa wake.
hashee

Picha 8 za Jumba la kifahari Oscar Pistorius alilopanga kuishi na mpenzi wake kabla ya kumuua.

 

oscar2
Hizi ni baadhi ya picha Jumba kubwa la kifahari la Oscar Pistorius lenye thamani ya Paundi 530,000 ambalo alipanga kuhamia na mpenzi wake Reeva Steenkamp kabla ya tukio la kumpiga risasi akiwa bafuni ambapo kesi yake bado inaendelea.
Pistorius tayari alikwishalipia nyumba hiyo baada ya makubaliano na mpenzi wake huyo baada ya kutembelea nyumba hiyo ambapo wapenzi hao waliwaambia marafiki zao juu ya mpango wa kuhamia katika nyumba hiyo jijini Johannesburg.
oscar1
oscar3

oscar4 

oscar5

oscar6

oscar7

oscar8

oscar9

Mrembo wa Kenya Mwenye Umbo la Utata Corazon Kwamboka, Akiri Kumzimia Hermy B


Kama girlfriend wako akikuona unaongea na Corazon Kwamboka, hakuna shaka kuwa roho yake itamdunda kwakuwa wazo la kwanza litakalomuijia kichwani ni kuwa himaya yake ipo matatani. Corazon Kwamboka ambaye ni mwanasheria by profession, ameiteka blogsphere ya Kenya kwa umbo lake matata na kuvutia kama la Agnes Masogange.

Hii imewafanya wasichana wengi wa Kenya wamuonee wivu na kumsema vibaya. Pamoja na kuwatoa wanaume udenda kwa umbo lake, producer wa B’Hits, Hermy B, amekuwa mwanaume mwenye bahati kwakuwa amezimiwa na mrembo huyo aliyeamua kuweka wazi kwenye Instagram.

“Before Monday ends.. here is my real crush #MCM. Hermes tpf,” aliandika mrembo huyo Jumatatu hii.

Kuhusu Young Dee kupigwa alipokwenda Skylight Band.


Screen Shot 2014-04-30 at 4.24.26 PM

Kama hukusikia hii inamhusu Young Dee na hii inasemekana kuwa alipigwa makonzi wakati tamasha la Skylight Band likiendelea ambapo Soudy Brown anaamplify taarifa hizi ambazo Young Dee nae amesikika akizizungumzia.
Bonyeza play kusikiliza.

KAJALA AWAJIBU WANAO MTUKANA INSTAGRAM "KANTANGAZE USIPONITANGAZA NITAKUTANGAZA"

 Baada ya kushambuliwa sana huko Instagram kuhusu urafiki wake na Wema haya ndo majibu yake

FANS ATTACK LUPITA NYONG'O ON INSTAGRAM, CALLS HER A "MONKEY"


Jamaa awa Wazungu ...Hawana hata aibu kumwita Binadamu Mwenzao hivyo ki ukweli hii imeniuma sana embu jionee

KWANINI MAMBO HUWAENDEA MRAMA WASANII WANAO JITOA TIP-TOP CONNECTIONS?


Wako wapi MB Dog, Z-Anto, Keisha, Pingu, Spark, Dongo Janja na wengine waliowahi kujitoa Tip Top Connection? Kuna nini Tip Top, kwamba ukijiondoa tu huwezi kufanikiwa mbeleni? Kwanini ni wasanii wachache tu, tena anaweza kuwa Cassim Mganga peke yake ambaye baada ya kujiondoa kwenye himaya hiyo yenye makazi yake Manzese jijini Dar es Salaam, amefanikiwa kuwa na career ya kueleweka? Wengine wote, wamefeli.. big time.

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa wengi wakiondoka hutoa maneno ya kashfa na hivyo kujikuta wakinyea kambi.

Hebu tuwaangalia hawa watatu, Dogo Janja, Z-Anto na MB Dog

Dogo Janja

Unakumbuka June 2012, kipindi Dogo Janja ameondoka Tip Top? Habari hiyo ilikuwa kubwa kiasi ambacho simu za Madee na Dogo Janja zilikuwa busy kwa interview. Kila pande ilikuwa ikiutupia lawama upande wa pili.

Kama umesahau wacha tukukumbushe ilivyokuwa.

Sababu zilizotajwa na Tip Top Connection ni kwamba Dogo Janja alilewa sifa na kuwa mtoro shuleni.
Kwa mujibu wa interview aliyofanya na Bongo5, uonevu na dhuluma ndivyo vilivyomchosha Dogo Janja kuishi Dar es Salaam na kujiondoa kwenye himaya hiyo.

Alisema tangu aje Dar es Salaam hakuwahi kusaidiwa chochote na Madee zaidi ya mambo ya muziki pekee huku kula, malazi na ada ya shule vikifanywa na rafiki yake Madee aitwaye Abdallah Doka ambaye (Dogo Janja) alikuwa akiishi kwake.

Alisema kutokana na ngoma zake kujipatia umaarufu alikuwa akipata show nyingi nchini na zote alikuwa halipwi chini ya milioni moja. Kilichokuwa kinamsikitisha anasema ni kulipwa hela kidogo isiyozidi laki mbili na hivyo kumfanya aishi kwa tabu licha ya kuingiza hela nyingi za show. “Nilikuwa navumilia tu bro kwasababu kila nilipolalamika kuhusu mambo ya hela Madee alikuwa mkali sana,” aliiambia Bongo5.

Dogo alidai ilikuwa inafikia wakati akifanya show za ukumbuni hulipwa elfu hamsini au chini ya hapo na wakati mwingine alikuwa halipwi kabisa. Alisema tamaa ilizidi kumwingia Madee kiasi cha kumnyang’anya kadi yake ya benki na kuanza kuchukua hela bila kujua password aliipata wapi. “Kuna wakati nilikuwa nataka kumtumia mama laki moja, Madee akanikataza eti kwakuwa watadhani nina hela sana,” alisema.

Aliongeza kuwa kuna siku Madee alimpigia simu na kumwambia kuwa kaka yake wa Kibaha ameandaa show ya CCM na angemlipa shilingi laki moja. “Hivi kweli bro mimi ni mtu wa kufanya show ya laki moja?” alihoji. Hata hivyo aliamua kukubali ili kuepusha lawama.

Baada ya show kumalizika alisema yeye na back up artist wake walirudishwa saa saba usiku wakati asubuhi yake alitakiwa kwenda shuleni kuchukua namba ya mtihani na kuandaa dawati la kukalia. Dogo Janja alisema kuwa ilimuuma sana kwakuwa muziki haujampa chochote licha ya Madee ambaye huwa hapati hata show kumtumia kimaslahi na hadi kufikia hatua ya kujenga nyumba yake.

“Ni kama vile Madee alinipanda ili anivune,” alisema.

Alifunguka kuwa hadi kufikia Tip Top watangaze kumfukuza alikuwa kwa Tundaman akipiga story na Madee akamuita kisha kuanza kumpiga na kwamba alichukua simu yake akaondoka nayo. “Jamaa alianza kujitumia meseji kutoka kwenye simu yangu kwenda kwake za matusi ama kuwa nataka kumroga. Jana nimemuonesha Milard hizo meseji na amesikitika sana.”

Alisema kitendo cha kumwambia Madee kuwa amechoka na anataka kurudi nyumbani ndicho kilimfanya amfanyie yote hayo hadi kumwambia kuwa watahakikisha wanambania asifanye vizuri tena kwenye muziki. Pia amedai kuwa Madee aliwapigia simu wazazi wake ili wamkataze Dogo Janja asifanye interview na vyombo vya habari.

“Wanajua nikiongea wataabika sana.”

Baada ya drama zote hizo ndipo Ostaz Juma akaingia kwenye picha. Alimtumia nauli ya ndege rapper huyo kutoka Arusha kurejea Dar na akajiunga na Mtanashati Entertainment ambayo wakati huo ilikuwa na heshima kidogo. Dogo Janja alipewa maisha, akalipiwa ada ya shule na kutoa ngoma iitwayo Ya Moyoni aliyomshirikisha PNC. Haikupita muda, mambo yakaanza kutokota.

Kwa mara nyingi Ostaz Juma alimfukuza na kumrejesha tena rapper huyo kwa madai kuwa hakuwa na nidhamu. Hata hivyo, imefika wakati ambapo Mtanashati Entertainment imekosa muelekeo na Dogo Janja anahisi meli inazama. Kuomba msamaha ili mambo yaende ni kitu kisichoepukika kwake kwakuwa ni kweli Dogo Janja wa ‘Mtoto wa Uswazi’ ft Godzilla amepotea kabisa.

Z-Anto

Ni ngumu kuamini ukubwa wa Z-Anto baada ya kutoa hit single yake ‘Binti Kiziwi’ ungekuja kuyeyuka kama barafu ikutanapo na jua kali. Enzi Binti Kiziwi inahit, hakuna msanii aliyekuwa na show nyingi kama Z-Anto. Hata hivyo, meneja wa Tip Top Connection aliwahi kudai kuwa kipindi hiki ndipo msanii huyo alianza kuota ‘majipu’ kwapani na kuanza pozi nyingi. Jambo hilo lilimkera Babu Tale kiasi cha kuamua kuifuta kabisa video mpya ya msanii huyo iliyokuwa inategemewa kumpeleka juu zaidi. Baada ya kuondoka Tip Top mpaka leo hii, Z-Anto si yule tena wa zamani na ukweli hali yake kimuziki ni mbaya.

“Nililazimika kushuka kwa sababu hiyo. Lakini nilipokuja kuzigundua zile njia nikaweza kupenya na ngoma binafsi nilijisimamia mwenyewe kwa kila kitu ambayo ndio hiyo Kisiwa cha Malavidavi,” Z-Anto alikiambia kipindi cha Mseto cha Radio Citizen ya Kenya hivi karibuni japo alidai kuwa hadi leo Babu Tale anamtaka arejee kundini.

“Mpaka kesho (Babu Tale) bado ananipenda. Hata ukimuuliza katika wasanii wake anaowapenda atatajwa wawili asishindwe kunitaja mimi.”

MB Dogg

Unazikumbuza Latifa na Si Uliniambia? Hizo ni miongoni mwa nyimbo bora za Bongo Flava za muda wote lakini yuko wapi MB Dogg? Kama ilivyokuwa kwa Z-Anto, naye baada ya kujitoa Tip Top, mambo yalienda mrama. Ilimchukua miaka mingi MB Dogg kuweka ‘ego’ pembeni na kukubali kuwa kweli amepotea na anaiihitaji Tip Top kiasi cha mwaka huu kuweka mambo sawa na Babutale.

“Lakini kwa sasa nataka tumuangalie Mb Dogg kwa macho mawili,” Tale aliiambia Millaayo.com hivi karibuni. Mb Dogg ana kipaji watu wanaujua uwezo wa Mb Dogg, Mb Dogg sio kama amepotea hapana ila hana uongozi anahitaji promo ya nguvu tu akipata hiyo anarudi kupiga hela kama zamani.”

Hata yeye mwenyewe MB hivi karibuni alikiri kuwa kufanya muziki bila kuwa na uongozi wa kukusimamia ni kazi bure.

“Tip Top nilitoka na ndio kitu ambacho kilinirudisha nyuma sana,” MB Dogg aliiambia Bongo5 March 17 mwaka huu.

“Pale nilikuwa nafanyiwa kila kitu, nilikuwa narekodi tu kazi yangu vitu vingine vyote wanafanya wao so baada ya kutoka na kujisimamia mwenyewe nikaanza kuyumba na kuhangaika huku na kule. Kwahiyo kitu ambacho nimegundua msanii bila management nzuri huwezi fika mbali asikwambie mtu. Msanii anahitaji kuongozwa, kushauriwa na mambo mengine. Sasa hivi nipo Tip Top tumeingia makubaliano mapya ya kazi ndio maana nashukuru Mungu ngoma yetu mpya ‘Umenuna’ inasonga kidogo kidogo mpaka kieleweke.”

Kinachowaumiza zaidi wasanii walioondoka Tip Top ni kwamba wasanii waliosalia mathalani Madee, wameendelea kufanikiwa zaidi. Mwaka jana pekee, Madee anadai kuingiza zaidi ya shilingi milioni 150 kwa single yake moja tu ‘Sio Mimi’. Meneja wa Tip Top, Babu Tale akishirikiana na Said Fela ndio walio nyuma ya mafanikio ya Diamond Platnumz, kwahiyo ni wazi kuwa Babu Tale ni ‘hot cake’ kwa sasa na ndio maana wasanii wa Tip Top waliojiondoa wako radhi kumuomba msamaha ili warejee kundini.

Swali ninalokuacha nalo msomaji ni Je! Haiwezekani msanii aliyejiondoa Tip Top kuwa na career yenye mafanikio?

PENZI LA MR BLUE LAENDELEA KUMTESA NAJ.."TOKA NIACHANE NAE SIJAPATA MTU KAMA MR BLUE"

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya ambaye huwa anaishi na kufanya Kazi nchini Uingereza Naj amefunguka kuwa Tangu aachane Mr Blue zaidi ya Mwaka mmoja na miezi kadhaa iliyopita hajawahi kukutana na Mwanaume na wala hajawahi kumpenda mwanaume yeyote, Naj amefunguka hivi karibuni kabla hajaelekea U.K akaendelea kunitiririkia kuwa alikua na Mr Blue kwa miaka mitano na ikaishia kwa yeye kukimbiwa na Blue akamkana hadharani na kuanzisha mahusiano na mwanadada mwingine hali iliyomhuzunisha na kujutia muda wake, Naj akamalizia kwa kuniuliza Je angeutumia muda huo kwa kupiga kazi si angekua mbali sana? kwa hiyo sasa hivi anacho angalia ni kazi tu kwa kwenda mbele, yuko singooooooooooooo

UTAJIRI WA MTANGAZAJI DIDA GUMZO!....ATAJWA KUHUSIKA NA UUZAJI WA SEMBE

Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
AMINI usiamini lakini ndivyo ilivyo! Utajiri wa Mtangazaji wa Radio Times FM ya jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’ umeibua gumzo midomoni mwa watu wakidai kuna walakini juu ya upatikanaji wake.
Toyota Verossa ikiwa imepaki pembeni ya ghorofa analodaiwa kumiliki Dida.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Dida ana utajiri mnono lakini anafanya siri ili watu wasiulize alikoupatia kwa sababu si kwa njia halali.
NYUMBA MBILI, MOJA YA GHOROFA
Chanzo kiliendelea kudai kwamba mtangazaji huyo wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, ana nyumba mbili. Moja ipo Kigamboni na nyingine ipo Goba ambayo ni ya ghorofa  moja, zote jijini Dar.
“Ile ghorofa ya Goba ni kiboko. Ina uwanja mkubwa ndani kama wa mpira, kuna maegesho ya magari hata kumi. Kuanzia getini hadi mlango mkubwa kumesakafiwa,” kilisema chanzo.
Magari aina ya Toyota Carina na Verossa yote mali za Dida yakiwa yamepaki.
MAGARI MATANO YA KUTEMBELEA
Chanzo chetu kikazidi kwenda mbele kwa kudai kuwa mbali na umiliki wa nyumba, pia mwanadada huyo ana magari matano kwa ajili ya kutembelea tu.
“Mbali na nyumba hizo, Dida pia ana magari matano ambayo hubadili anavyotaka kwa ajili ya kutembelea tu kwenye mizunguko yake.
“Ana Toyota Verossa mbili, ana Toyota Noah rangi ya silva na nyeusi. Ana Toyota Vitz. Hivi karibuni ameanza mchakato wa kuingiza nchini gari lingine la sita aina ya Range Rover ‘Vogue’. Hebu fikirieni, Dida huyuhuyu mnayemjua, amepata wapi mali hizo?” kilihoji chanzo.
Khadija Shaibu ‘Dida’.
YADAIWA ANAUZA ‘UNGA’
Chanzo kilisonga mbele zaidi kwa kusema kuwa, habari za mitaani ni kwamba mtangazaji huyo anatuhumiwa kuuza madawa ya kulevya ndiyo maana ametajirika ghafla.
“Watu wamekuwa wakimsema kwamba fedha zake zinatokana na biashara ya kuuza unga. Si unajua wauza unga wana pesa sana?” kilisema chanzo hicho.
MADUKA MATATU YA NGUO
Katika tafutafuta, mapaparazi wetu waliwahi kuyanasa maduka matatu ya nguo za kike ambayo yapo Kinondoni, mmiliki wake akiwa ni Dida.
Katika mabango ya matangazo, maduka hayo yanasomeka; Dida Classic.
AMETOKA MBALI
Kabla ya kudaiwa kuwa na utajiri huo, wakati fulani Dida aliwahi kukumbana na misukosuko ya madeni ambapo benki moja maarufu jijini Dar es Salaam ilifilisi samani za sebuleni, nyumbani kwake Kinondoni, Dar baada ya kushindwa kulipa mkopo.
Dida akipozi jirani ya gari aina ya Range Rover Vogue alilopanga kulidondosha Bongo.
DIDA ASAKWA
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mapaparazi wetu walimtafuta Dida ili kueleza ukweli ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi sipendi kuanika vitu nilivyonavyo au ninavyomiliki ila ni kweli nina nyumba mbili, moja Kigamboni na nyingine Goba ya gorofa.
KUHUSU MAGARI
“Magari ninayo matatu na si matano, hilo Vogue mchakato unaendelea, ukikamilika nitaliingiza nchini.
MIRADI YA DUKA
“Kuhusu miradi yangu mingine siwezi kuianika hadharani kwa sababu, kwanza sipendi kabisa mambo hayo,” alisema Dida.
Toyota Noah kama anayomiliki Dida.
NI KWELI ANAUZA UNGA?
“Watu wamekuwa wakiongea sana kwamba nauza unga kitu ambacho si kweli, kwanza sijui hata huo unga unafananaje! Ila mimi ninajituma sana kwenye kazi pamoja na kufanya biashara mbalimbali.
“Sitasahau siku ambayo watu walikwenda kutoa taarifa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Dar) kuwa siku hiyo nasafiri na mzigo wa madawa ya kulevya.
“Nilipofika uwanjani nikawekwa chini ya ulinzi na kupekuliwa. Kama haitoshi nilipelekwa Hospitali ya Temeke (Dar) nikafanyiwa X-ray, hawakuona kitu ndipo nikarudishwa uwanja wa ndege kuendelea na safari
“Mimi nawaacha tu waongee watachoka kwa sababu hawajui wanachokifanya, ila mimi najitambua na kile ninachokifanya,” alisema Dida.
Toyota Vitz kama ya Dida.
Akaendelea: “Nilichokuja kubaini ni kwamba kuna wabaya wangu ndiyo walipeleka taarifa za uongo pale uwanjani. Wote huo wivu tu hakuna lingine.
“Kuanzia hapo nikaamua kufanya mambo yangu kimya-kimya, hakuna sababu ya kutangaza kwani wabaya ni wengi, wazuri wachache na si kila anayeku-chekea ni mzuri kwako.”
Source:GPL

Huu Ndio Mjengo wa Kifahari Anaoujenga Msanii Diamond Platinumz.

Diamond aonyesha mjengo wake anaoujenga na ulipofikia mpaka kwa sasa, tazama hapa picha uone jinsi ilivyofikia

VICTORIA KIMANI AAMUA KUACHIA PICHA ZA TATOO ALIZOJICHORA MPAKA SEHEMU ZA SIRI




Victoria Kimani ameamua kujipamba na urembo wa Pwani kwa kujichora na tattoo za Henna.

MASTAA WENYE NYOTA ZA NGONO!


Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Makubwa! Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahya ameanika nyota za baadhi ya mastaa wa Bongo katika kipengele cha mapenzi au ngono, Risasi Jumamosilimesheheni.
Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahya.
Akizungumza na mapaparazi wetu katikati ya wiki hii ofisini kwake Magomeni-Mwembechai jijini Dar, Maalim alitumia saa kadhaa kuangalia nyota ya mmoja baada ya mwingine na kueleza sifa zao katika sekta ya uhusiano na tendo la ndoa.
Wema Sepetu.
Baadhi ya mastaa alioweza kuwasoma nyota zao kirahisi ni pamoja na ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, waigizaji Wema Sepetu, Vincent Kigosi ‘Ray’, Aunt Ezekiel, Steven Jacob ‘JB’, Jacqueline Wolper, Blandina Chagula ‘Johari’ na wengine.
ALIANZA NA WEMA
Akimzungumzia Wema aliyezaliwa Septemba 28, Maalim alisema nyota yake ni Mizani hivyo ana tabia zifuatazo katika masuala ya mapenzi:
“Kwanza yeye (Wema) na Diamond nyota yao ni moja hivyo mambo yao mengi yanafanana.
“Wanapenda kuwa kwenye ulimwengu wa mapenzi na mahaba wakati wote. Wanathamini sana masuala ya ngono kuliko maisha mengine.”
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Wema Sepetu katika pozi la kimahaba.
NDOA NA DIAMOND
“Hawa watakuwa watu wa kuachana na kurudiana mpaka watakapofunga ndoa ya kifahari hapo baadaye.
“Kuhusu mambo mengine kinyota ni kwamba wana sifa ya uongozi, wanapenda kuwa huru na kujitegemea. Wanapenda kuheshimika kwenye jamii na ni wacheshi, wana hekima na diplomasia.”
Vincent Kigosi ‘Ray’.
KUHUSU RAY
Kwa upande wake Ray ambaye amezaliwa Mei 28, Maalim alisema nyota yake ni Mapacha.
Akimchambua kinyota kuhusu masuala ya mapenzi, alisema:
“Akimpenda mwanamke ana uwezo wa kumpa chochote, kimawazo na kila kitu, anaweza hata kuhamia nyumbani kwa mwanamke huyo.
Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mpenzi wake Chuchu Hans.
“Ila ni mtu anayechoka haraka na hawezi kudumu kwa muda mrefu kwenye penzi na mwanamke mmoja tu.
“Pia anapenda kuwa na mapenzi ya siri siku zote. Hata akioa ni lazima ataendelea kuwa na mwanamke wa nje ‘nyumba ndogo’.
“Mbali na masuala hayo, ni mtu mwenye hisia kali sana ambapo hukasirika upesi. Ni mtu mwenye uwezo wa kujieleza na kuzungumza, ana ushawishi mbele za watu.”
Aunt Ezekiel.
AUNT EZEKIEL NAYE
Akimchambua Aunt Ezekiel ambaye alizaliwa Oktoba 27, mtabiri huyo alisema nyota yake ni Nge.
“Kinyota, ni mtu mwenye ‘muwashawasha’ wa mapenzi, anapokuwa na hasira tu hupenda kuzimaliza kwa kufanya tendo la ndoa.
“Ni msiri sana. Ana wapenzi wengi lakini kwa siri. Kwake tendo la ndoa ni ishu muhimu sana katika maisha yake hasa ikizingatiwa kuwa, nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.
“Kwa mwenye moyo mdogo, asifanye mapenzi na mtu mwenye nyota hii kwani atajuta maisha yake yote. Lakini hayumbi na hakubali kushindwa hata kwa jambo ambalo halitamharibia popote.”
Jacqueline Wolper.
JB & WOLPER
Kwa upande wa JB aliyezaliwa Desemba 4, Wolper aliyezaliwa Desemba 6, Maalim alisema wote wana nyota moja inayofanana ya Mshale. Anaichambua nyota hiyo hivi:
“Wanapenda kufanya ngono kwa muda mrefu, hivyo mwanamke au mwanaume atakayekuwa nao kimapenzi lazima awe amekula akashiba vizuri kabla ya tendo lenyewe.
Jacob Steven ‘JB’.
“Wapenzi wao wanapowaonesha dalili ya kuwapenda sana basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu.
“Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu na wanakolea vilivyo. Mara nyingi wanapenda sana kuwa na wapenzi wapya, lakini hawapendi mapenzi ya kudumu kwa sababu yanawanyima uhuru.
Blandina Chagula ‘Johari’.
NYOTA YA JOHARI SASA
Akimzungumzia Johari aliyezaliwa Agosti Mosi, mtaalam huyo alisema nyota yake ni Simba. Anasema:
“Kinyota ana tatizo la kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani ni mtu anayeumia.
“Mara nyingi hujipa hisia za kupendwa na mpenzi wake kama anavyompenda yeye.
“Ni mkarimu lakini ni jeuri, anapenda sana kuonea wenzake. Anapenda kujionesha na humharibu mpenzi wake.”
Credits:Global Publishers

WHEAT CLICK THIS PHOTO