Slider[Style1]

HABARI

BONGO MOVIES

BONGO FLEVA

.

BONGO VIDEOS

Style5[ImagesOnly]

STORY ZA INSTAGRAM

RIDHIWANI KIKWETE "SIASA NINAZO FANYA HAZINA UHUSIANO NA BABA YANGU"

Chalinze. Mshindi wa kura za maoni za kugombea ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Kikwete amesema siasa anazofanya sasa hazina uhusiano wala ubia na baba yake.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura za maoni za chama hicho katika jimbo hilo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Msata alisema anafanya siasa kwa maisha yake na si kwa mgongo wa baba yake kwani aliingia katika siasa akiwa na umri wa miaka mitano na hakuwahi kufanya hivyo kwa sababu ya baba yake.

“Siasa ninayofanya haina uhusiano na baba yangu, nafanya siasa kwa maisha yangu na sina ubia na baba yangu katika hili” alisema mtoto huyo wa Rais Jakaya Kikwete.

Akijibu swali la kwa nini amejiingiza katika siasa tofauti na maneno yake aliyowahi kutamka mwaka 2010 kuwa hawezi kushiriki katika kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo hilo, Ridhiwani alisema wakati huo hakuwa tayari.

“Kwenye siasa usiwe muwazi katika kila kitu, ukiwa hivyo unawapa nafasi maadui kukushambulia, mimi hapa Chalinze ni kwetu, kwa wazazi wangu na kule Bagamoyo tunakwenda tu kikazi na ndiyo maana nikaamua kurudi nyumbani kuomba ridhaa. Nashukuru kuongoza katika kura za maoni ninaona ni kiasi gani ninaungwa mkono,” alisema.

Katika kura hizo za maoni Ridhiwani alibuka mshindi kwa kura 758, akifuatiwa na Imani Madega aliyepata kura 335, Ramadhan Maneno (206) na Mkwazu Changwa (17).

Kamati Kuu ya CCM (CC), inatarajiwa kukutana Machi 8, mwaka huu k

SEREKALI KUMLIMA BARUA BALOZI WA CHINI BAADA YA KUJIHUSISHA NA CCM

Dar es Salaam. Serikali imesema mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wanapaswa kutambua kuwa, wanawajibika kuheshimu Mkataba wa Kimataifa wa Vienna unaoainisha taratibu za diplomasia.

Pia, inasema inajiandaa kumwandikia barua Balozi wa China nchini, Lu Younqing kutokana na hatua yake ya kujihusisha na mambo ya siasa.

Wiki iliyopita, Balozi Lu alijitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mkoani Shinyanga, huku akiwa amevalia moja ya sare za chama hicho, hatua ambayo imezusha mjadala miongoni mwa vyama vya siasa na wachunguzi wa mambo ya kidiplomasia.

Akizungumzia kitendo hicho jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, alisema Serikali inajiandaa kumwandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kwamba itafanya hivyo baada ya kukusanya taarifa zake.

Hata hivyo, Mahadhi alisema Tanzania na China zitaendelea kuwa marafiki wanaoshirikiana kwenye nyanja mbalimbali kwa shabaha ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.

“Hizi taarifa za balozi kuwa kwenye mkutano wa CCM nami zimezisikia na kuziona kwenye vyombo vya habari, tunachokifanya sasa wataalamu wetu wanaendelea kuzifanyia kazi, baadaye tutamwandikia barua kumkumbusha wajibu wake,” alisema.

Alisema siyo vyema kwa mabalozi kushiriki mambo ya kisiasa, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na Mkataba wa Vienna ambao ndiyo unaotoa mwongozo.

Pia, Mahadhi aliasa vyama vya siasa kutoachia majukwaa yao yakitumiwa na wanadiplomasia, akieleza kuwa navyo vinawajibika kuheshimu mkataba huo.

Alisema iwapo pande zote zitaheshimu mkataba huo, hakutakuwa na kurushiana lawama.

Mwananchi

CCM YAFUKUZA MADIWANI 8 WA MANISPAA YA BUKOBA

 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera, leo kimewafukuza madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kupitia chama hicho na kufutwa nyadhifa zao za udiwani kutokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea

NCHEMBA ATUHUMIWA KUSHUSHA HESHIMA YA CCM MBELE YA UMMA NA KUCHANGIA MATOKEA MABAYA


MATUKIO kadhaa ya kisiasa, mwelekeo, kauli na mienendo ya baadhi ya wanasiasa waandamizi na wenye nguvu katika Chama cha Mapinduzi (CCM) vimeibua mkanganyiko na hali tete ndani ya chama hicho, Tanzania Daima Jumamosi limebaini.

Kwa muda sasa, kumekuwa na minyukano ya ndani kwa ndani miongoni mwa viongozi waandamizi wa CCM, huku baadhi yao wakilaumiana kwa “kuchafua na kuua” chama.....

WHEAT CLICK THIS PHOTO