Posted by: ujugu
Posted date: 21:10
/
Burudani
Producer wa wimbo mpya wa Ben Pol,
‘Unanichora’, Fundi Samwel ambaye ni raia wa Sweden, amethibitisha
kuachana na mke wake, Saraha.
Mtayarishaji huyo amesema sababu kubwa
ya kuachana ni ubusy waliokuwa nao uliosababishwa na muziki na hivyo
kuwafanya wasiwe karibu kwa kipindi kirefu.
“Mimi na Saraha tuliachana, kilikuwa
kitu kibaya kwangu na kwake pia ndio maana nilikuwa kimya kidogo mwaka
huu sababu unajua moyo ulivunjika sana na mood lazima ipotee,” Fundi
Samwel amemuambia Sam Misago kwenye kipindi cha Power Jams cha East
Africa Radio.
“Unajua kukaa na kufanya muziki lazima
utumie muda sana na unatumia akili sana, na hata yeye alifanya kazi
nzuri hapa, alikuwa busy sana, namimi nilikuwa busy ya studio. Unajua
anakuta foleni kila siku halafu wewe unapiga kazi kama masaa 15 hivi and
then unachoka sasa huwezo kuongea vizuri. Hata Saraha alichoka, unajua
tulishindwa kuongea vizuri na kitu kiliendelea. And then tulipofika
Sweden, unajua upendo uliisha tu, uliisha kabisa,” aliongeza.
Samwel ambaye tayari amerejea kwao nchini Sweden amesema yupo Tanzania kwa wiki mbili kutengeneza nyimbo kadhaa.