Slider[Style1]

HABARI

BONGO MOVIES

BONGO FLEVA

.

BONGO VIDEOS

Style5[ImagesOnly]

STORY ZA INSTAGRAM

NMB leo imefungua tawi jipya katika mji maarufu wa Kibaigwa –Dodoma. Tawi hilo litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya NMB nchini kote.
Tawi la Kibaigwa limefunguliwa na Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, Mh Job Ndugai.
Kufunguliwa kwa tawi la Kibaigwa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wa NMB wa eneo hilo wa kupata tawi lenye nafasi ya kutosha .Aidha  eneo hili ni karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wakubwa wa NMB na wananchi kwa ujumla .
Kwa kutambua pia nia ya kuendelea kuchangia huduma mbali mbali za kijamii, benki ya NMB inatoa shilingi Milioni 10 kwa ajili ya hospitali na shule kama shukrani za Benki kwa wananchi wa Kibaigwa kwa kuendelea kwao kuunga mkono maendeleo ya benki.
NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 150, ATM Zaidi ya 500 nchi nzima pamoja na idadi ya wateja inayofikia Milioni mbili hazina ambayo hakuna benki yenye nayo.

 Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Mhe.Job Ndugai ,akiweka sahihi
kwenye kitabu cha wageni mara tu baada ya uzinduzi wa Tawi la NMB kibaigwa .
Hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo umefanyika jana katika viwanja vya Tawi la NMB Kibaigwa Wilaya ya Kongwa mkoni Dodoma
 Sehemu ya wageni Waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
 Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Mhe.Job Ndugai  akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kibaigwa
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Mhe.Job Ndugai (Kati kati)akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kibaigwa.

About ujugu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

WHEAT CLICK THIS PHOTO