Unapozungumzia kifo hakuna mwanadamu yeyote duniani ambaye atapenda kusikia ama kutaka kujua atakufa lini na ni kawaida kila mmoja huwa anaogopa anaposikia taarifa zinazohusiana na kifo.
Lakini kwa mzee Muhashta Murasi
ambaye alikuwa fundi viatu aliyestaafu kazi hiyo mwaka 1953 akiwa na
umri wa miaka 122, amesema anakisubiri kifo kwa hamu kubwa sana kwani
amechoka kuishi.
Kwa sasa ana umri wa miaka 180 na
alizaliwa mwaka 1835 na tayari ameingia kwenye kitabu cha dunia cha
kumbukumbu cha Guines kwa kuwa ndiye binadamuu pekee mwenye umri mkubwa
kuliko wote.
Alizaliwa katika mji wa Bangalore, India
na kwa mujibu wa daktari aliyekuwa akimfanyia vipimo amedhibitisha kuwa
amekua hana magonjwa ya mara kwa mara hali inayochangia kuendelea
kuishi kwa muda mrefu.
Lakini mtandao wa World News Report umesema huenda habari za mzee huyo hazina ukweli wowote.
No comments: