Masanja mkandamizaji mchekeshaji kutoka kundi la Komedi Orijino
kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika mawazo yake juu ya uhusiano
wa Wema Sepetu na Diamond.
Hiki ndicho alichoandika,”Hili swala la diamond na wema nadhani mungu
amemuhurumia mmoja wapo kati ya hao wawili. Kama wangekuwa watu wa
kuoana wangesha oana uchumba gani mrefu kama wanasomea udokta????
Rafiki yangu nasib, kama kweli mlipendana kwa dhati hizo kasoro
zinarekebishika, maana hakuna mwanadamu aliye sahihi kwan hata ww nasib
unamapungufu yako. Na wewe dada yangu wema lazima ujue mme ndio kichwa
cha nyumba kwa maelezo hayo inaonyesha haumsikilizagi mwenzio omba
msamaha tenaaa na tena na ukubali kubadilika.
Mi sipendi mkiwa mnaongozana wote kwenye ma show ya usiku mme kafanye
kazi mke abaki home ukirudi mwili umepoa hata ujauzito unaingiaa!! Sasa
woote stejini mkirudi miili ya moto si mtazaa popompoo jamaniii!!
Nitafurahi kusikia tofauti zenu mmezimaliza kwa amani ili mashabiki wenu
wasijisikie vibaya
Soma alichoandika Masanja Mkandamizaji kuhusu uhusiano wa Wema na Diamond

No comments: