Wakati bado kuna maswali mengi kuhusu
magaidi waliohusika na shambulio la Westgate kama kweli waliuawa kama
isemavyo taarifa ya serikali ya Kenya, mtandao wa Mirror umetoa taarifa
kuhusu tetesi za uwezekano wa magaidi hao kutorokea njia ya maji taka
kutoka katika jengo hilo.
Mtandao huo umedai kuwa baadhi ya
magaidi walitoroka kupitia njia ya maji taka iliyoko chini ya jengo la
Westgate inayoenda kutokea katika mto Nairobi.
Kwa mujibu wa habari hiyo njia hiyo
inaanzia eneo la maegesho ya magari katika jengo la Westgate na inaenda
moja kwa moja kutokea katikati ya jiji la Nairobi. Magaidi hao
wanahofiwa kutumia njia hiyo ya maji taka kutoroka na kuwaacha wengine
wakiendelea kushambulia.
Taarifa hiyo inaendelea kudai kuwa wana
usalama wanadai kuwa magaidi wa Al-shabaab walisafiri umbali wa nusu
maili kwa magoti katika njia hiyo ya chini ya ardhi katika njia ya maji
taka.
Chanzo kimoja kilisema “They escaped
like sewer rats. The terrorists would have been able to pass through the
underground tunnels at a rapid pace and surface almost unnoticed”.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa
wachunguzi wa Kenya hawakuigundua njia hiyo ya kutorokea mpaka masaa 72
kupita baada ya shambulio kutokea.
Hapa ndipo inapotokea njia hiyo ya maji taka kutoka Westgate hadi katikati ya jiji la Nairobi |
No comments: