MWALIMU wa Shule ya Msingi Morotonga, wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara,
Karata Mugunda, anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani hapa, kwa
tuhuma za kumpiga na kumlisha kinyesi mtoto wake wa kumzaa mwenye umri
wa miaka 10.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu, Wilaya ya Serengeti, Samwel Mewama, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba mtoto huyo alilishwa kinyesi alichokuwa amejisaidia
ndani ya nyumba yao.
Kwa mujibu wa Mewana, tukio hilo la kusikitisha lilitokea Agosti 14, mwaka huu saa 12 alfajiri.
“Chanzo
cha tukio hili la kikatili ni mtoto huyo kujisaidia haja kubwa ndani ya
nyumba, baada ya kuogopa kutoka nje usiku wa manane.
“Baada ya
kujisaidia, baba yake ambaye ni mwalimu, alikasirika na kuamua
kumwadhibu kwa kumchapa fimbo sehemu za makalio na kumsababishia
majeraha ya kutisha.
“Pamoja na kumwadhibu kwa fimbo,
alimlazimisha ale kinyesi chote alichojisaidia kisha akamlazimisha anywe
maji kwa wingi,” alisema Mewana.
Akizungumzia jinsi alivyopata
taarifa za tukio hilo, alisema ofisi yake ilipigiwa simu na mwalimu
mmoja anayefundisha shule moja na mtuhumiwa.
Baada ya taarifa hiyo, alifuatilia ili kujua ukweli wake ndipo alipomkuta mwanafunzi huyo akiwa amejeruhiwa vibaya makalio yake.
“Kwa
kweli nilimkuta ana hali mbaya, kwa hiyo nilichokifanya nilimchukua na
kumpeleka Kituo cha Polisi Mugumu nikapewa PF 3 kwa ajili ya matibabu
hospitalini,” alisema.
Aliongeza kwamba, baada ya polisi kupata
taarifa hiyo na kushuhudia majeraha aliyokuwa nayo mwanafunzi huyo
kupitia dawati lao la kijinsia, walikwenda kumkamata mwalimu huyo ili
hatua zaidi ziweze kufuata.
Daktari wa Zamu katika Hospitali ya Nyerere DDH, Dk. Ohoka Joseph, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.
Alisema mtoto huyo alijeruhiwa vibaya kwenye makalio yake na kwamba ameathirika kisaikolojia.
“Huyo
mtoto ameathirika kisaikolojia, kwa hiyo, kuna haja akafanyiwe
uchunguzi kutokana na athari za kipigo na tukio alilofanyiwa.
No comments: