Baada
ya usajili wa Ander Herrera na Luke Shaw, Manchester United
wamekamilisha usajili wa mchezaji mwingine ambae ni Marcos Rojo, beki wa
kiargentina aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Sporting Lisbon.
Rojo ambaye alichaguliwa katika kikosi bora cha kombe la dunia,
amejiunga na United kwa ada ya uhamisho wa £16 pamoja na Luis Nani
kwenda Sporting kwa mkopo ambapo pia Manchester United wanaripotiwa
kuhamishia nguvu zao kwa Angel di Maria wa Real Madrid.
Unaambiwa Man United wamekamilisha usajili mwingine wa huyu Muargentina.

No comments: