Wazazi
wa wasichana waliotekwa nyara nchini Nigeria wamekanusha madai kuwa
wanaingiza siasa kwenye kilio chao kuitaka serikali ya nchi hiyo iwaokoe
watoto wao.
Hii ni baada ya wazazi hao kukataa wito wa kukutana na rais Goodluck
Jonathan hapo jana baada ya kushinikizwa na mwanaharakati mdogo kutoka
Pakistan Malal Yousafzai.
Rias Jonathan amesema ni aibu kubwa kwa wazazi hao kuruhusu
kushinikizwa na mitandao ya kijamii hasa kutokana na kampeni yao kwenye
mitandao yenye kauli mbiu, “Bring Back Our Girls”.
Lakini msemaji wa wazazi hao, amesema kuwa walikataa kukutana na Rais
kwa sababu jamii ya watu wa Chibok haikuwa imewapa ruhusa kufanya
hivyo.
No comments: