Baada ya uwepo wa tetesi za kuihama Liverpool kushika hatamu kwa
takribani wiki 3 sasa, hatimaye leo hii Luis Suarez amejiunga rasmi na
FC Barcelona akitokea Liverpool.
Usajili wa Suarez umeigharimu FC Barcelona kiasi cha £65m kwa mujibu
wa mtandao wa Barcelona, na hii ni rekodi kwa Liverpool – Suarez anakuwa
mchezaji aliyeuzwa kwa fedha nyingi zaidi na klabu hiyo iliyoshika
nafasi ya pili kwenye EPL msimu uliopita.
Suarez ambaye alijiunga na Liverpool akitokea Ajax, pia ameweka
rekodi ya kuwa mchezaji anayeshika nafasi ya nne kwa kusajiliwa kwa
fedha nyingi zaidi nyuma ya Bale, Ronaldo na Neymar.
Hata hivyo pamoja na usajili huo mchezaji huyo hatoweza kuitumikia
Barca mpaka adhabu yake ya kufungiwa mechi 8 na kifungo cha miezi 4
kitakapoisha.
Usajili wa Luis Suarez FC Barcelona na rekodi mpya ya gharama za usajili

No comments: