
Kesi hizo za udhalilishaji kwa kusambaza
picha za utupu, vitisho, ununuzi/uuzaji wa binadamu, udanganyifu, na
vitisho zimefunguliwa kwenye mahakama moja jijini Yaounde, Cameroon, na
aliyekuwa mchumba wa mshambuliaji wa huyo za zamani wa Chelsea, Hélène
Nathalie Koah.
Mapema wiki iliyopita Koah alifungua kesi hizo dhidi ya Eto’o ambaye amekana mashtaka hayo.
Hatua hiyo ya imekuja siku chache baada ya
kusambaa kwa picha zake za utupu kwenye mtandao Facebook, ambazo mhudumu
huyo wa zamani wa ndege amesema zimesambazwa na Eto’o aliyekuwa mpenzi
wake.
Eto’o amekanusha kuhusika na mchezo huo
mchafu, na katika kujibu mapigo mchezaji huyo anayeongoza kwa kutwaa
tuzo nyingi za uchezaji bora barani Afrika, amefungua kesi ya matumizi
mabaya ya fedha($410,755) alizompa Ms Koah kwa ajili ya kufungua taasisi
ya kusaidia jamii wakati walipokuwa wapenzi.
Mwanamke huyu alishawahi kuwaingiza kwenye beef mwanamuziki Fally Ipupa na Eto’o kwa kuwachanganya kimapenzi.
No comments: