Slider[Style1]

HABARI

BONGO MOVIES

BONGO FLEVA

.

BONGO VIDEOS

Style5[ImagesOnly]

STORY ZA INSTAGRAM

KWAKO, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’. Naamini u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Kwa upande wangu nipo sawa, nakimbizana na maisha.
Nina machache ya kukushauri kuhusiana na maisha yako kama staa ambaye kwa sasa umetangaza kuokoka. Kwa maneno mengine ni kwamba, umeondoka kwenye utaifa, upo mikononi mwa Muumba wako.Nimekufahamu kwa kitambo kidogo. Kwangu mimi, wewe ni mmoja wa mastaa wa ukweli katika uchekeshaji Bongo. Mwenye kipaji cha hali ya juu na unayejua unachokifanya.
Tatizo ni kwamba, nashangazwa na aina ya maisha yako baada ya kutangaza kuokoka. Ninavyojua mimi, kuokoka ni kuachana na maisha ya awali ambayo (pengine) yalikuwa hayampendezi Mola na kugeukia katika maisha safi.Niliposikia umeokoka nilifurahi kuona kuwa umeelekea sehemu sahihi zaidi kiimani. Lakini moyoni nilikuwa na shaka kidogo maana wapo wasanii wengi kwenye uigizaji ambao walitangaza kuokoka lakini baadaye wakaonekana kwenye njia zao za awali.
Ukiachana na waigizaji, pia kuna wasanii wa Bongo Fleva ambao nao waliingia kwenye ulokole na mara wakaamua kurudia maisha yao ya awali.Baadaye  nikasikia kuwa unasomea Uchungaji (ingawa inaelezwa kuwa ni Uinjilisti), hapo sikuwa na shaka tena na wokovu wako. Niliamini kwa mtu ambaye ameamua kuingia kwenye kufundisha wengine njia iliyo sahihi hawezi kudanganya kuwa ameokoka.
Siyo kama naingilia maisha yako au nakukosoa kwenye suala la imani yako. Uzuri ni kwamba, nami ninaamini katika imani yako, hivyo sioni tatizo kukushauri.Tatizo lipo kwenye staili yako ya maisha. Ni kweli kwamba umeokoka, lakini itawezekana vipi usuke mabutu kichwani? Maandiko yanaeleza wazi kuwa, wanaoamini ni barua inayosomeka kwa watu wote.
Je, watu watasoma nini kupitia mabutu? Unaweza kusema kuwa, imani ya mtu iko moyoni, hapo sitakubaliana na wewe, maana kinachoonekana nje, kinawakilisha kilichomo ndani.Vipi kama kanisa zima, wanaume wataingia  wamesuka? Nafikiri si jambo sahihi. Watu watapata shaka na wokovu wako, tena mchunga kondoo. Wengine wanaweza kuona wokovu si jambo ‘serious’. Kwamba mtu anaweza kuingia na akaendelea na mambo yake yaleyale, jambo ambalo si la kweli.
Wokovu ni pamoja na mwonekano wa nje. Mavazi, mitindo ya nywele n.k.Jambo jingine ambalo limenishangaza ni namna unavyoingiza komedi kwenye mambo yanayohusu dini.Usahihi wa kufanya utani kwenye vichekesho huku ukitaja jina la Mungu unatokea wapi? Masanja tumezuiwa kufanya mzaha au kulitaja bure Jina la Mungu wetu.
Nakushauri kama ni kweli umeamua kuokoka, badilika lakini kama unahisi bado unatamani maisha ya kawaida na kujichanganya, chagua moja ili jamii isikutafsiri tofauti.Ni uamuzi wako kufuata au kuacha hapahapa, lakini la muhimu ni kwamba, nitakuwa nimeshakushauri. Ubarikiwe sana mpendwa!
Yuleyule,
Mkweli daima,
.........................
Joseph Shaluwa.

About ujugu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

WHEAT CLICK THIS PHOTO