Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani katika Mkoa
wa Dar es Salaam
yatafanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Temek
e katika Viwanja vya
Mwembeyanga, ambapo uzinduzi utafanyika tarehe 6/03
/2014 na kilele
itakuwa ni siku ya Jumamosi tarehe 8/03/2014.
Chimbuko la Siku ya wanawake Duniani lilianza miaka
mingi na mtakumbuka
mwaka 1911 Wanawake kule Nchini Marekani waliandama
na kudai haki zao
ambazo walikuwa wakizikosa kama vile:
kulipwa ujira mdogo,
kufanyishwa
kazi ngumu na kwa
masaa mengi,
kukosekana kwa huduma za jamii na
ubaguzi wa kijinsia. Mara baada ya Umoja wa Mataifa
kuanzishwa mwaka
1945,
lilipitishwa azimio kwamba tarehe 08 Machi ya kila
mwaka iwe ni Siku
ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani.
Kwa hiyo, wanawake wote duniani wanaadhimisha siku
hii kwa
kukumbushana kwa ajili ya kuweka mikakati zaidi ya
kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazowahusu Wanawake
.
Miongoni mwa
changamoto hizo ni wanawake kutopewa haki sawa kati
ka ngazi za maamuzi
na kutoshirikishwa.
Wanawake katika jamii hutoa mchango
mkubwa katika
kutunza familia,
lakini bado wanaathirika zaidi na maradhi kama
vile
UKIMWI,
vifo vinayotokana na uzazi, kupigwa, kunyimwa haki
ya kumiliki
mali, n.k . Hivyo,
maadhimisho haya si kwa ajili ya kufanya sherehe t
u,
bali
pamoja na
kufanya tathimini namna gani tumepiga hatua, tuko p
alepale au
tunadidimia.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu 2
014 yataongozwa
na kauli mbiu,
“Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia”.
Ujumbe
huu unaelimisha na kuhamasisha jamii ielewe umuhimu
wa kuyapa
kipaumbele masuala ya Kijinsia ili kutoa fursa sawa
katika Maamuzi kati ya
Mwanamke na Mwanaume na hatimaye kuleta usawa katik
a ngazi zote za
kijamii, kisiasa, kiuchumi na kutoa fursa sawa kati
ka shughuli zote za taifa hili.
Hivyo ni jukumu la wanawake na wanaume kushikamana
na kudumisha
usawa ndani ya familia ambako ndiko chimbuko la mas
uala yote ya
mabadiliko na usawa wa kijinsia yanakoanzia.
No comments: