MAKALI YA KILIMANJARO STARS YAIPA TEAM YA KENYA MCHECHETO-LAZIMA WAKAE
Kenya itacheza na Stars kesho Jumanne kwenye mechi ya nusu fainali ya Chalenji kwenye Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.
Awali nusu fainali hiyo ilikuwa ichezwe hapa Mombasa, lakini kutokana na hali ya joto ambayo inaibeba Tanzania na kukaa vibaya kwa wachezaji wa Kenya wanaoishi Nairobi kwenye baridi ndio maana mechi hiyo imeahirishwa.
Baada ya mechi dhidi ya Rwanda ambapo Kenya ilishinda bao 1-0, Adel alikiri kwamba; “Hali ya hewa ya Mombasa si nzuri kwetu ni joto kiasi na wachezaji wangu hawajazoea.”
Habari za ndani zinadai baada ya Uwanja wa Kisumu kushindikana kumalizika kwa wakati waandaji walipanga mechi za nusu fainali zichezwe Mombasa na fainali ikachezwe Nyayo mjini Nairobi lakini kwa hali waliyoiona katika mechi za juzi Jumamosi wenyeji wakaamua kupeleka mechi ya Stars Machakos. Mechi nyingine ya nusu fainali itachezwa mjini Mombasa.
Habari za ndani zinadai kwamba Adel amewaambia viongozi wake kwamba endapo Kenya ikicheza na Stars mjini Mombasa itakuwa kwenye wakati mgumu kutokana na Tanzania kuzoea hali ya joto na vilevile ina sapoti kubwa Mombasa kwavile ni jirani na Tanga.
Kenya iko kwenye presha ya kufuzu fainali kwani siku ya fainali nchi hiyo itakuwa ikisherehekea Jubilee ya miaka 50 ya uhuru wake.
Wakati huohuo, Zambia iliitoa Burundi kwa penalti 4-3 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika jana Jumapili hivyo kutinga nusu fainali.
No comments: