Hiki
ndicho walichokisema mashabiki hawa wa Simba ‘Leo hii unakuta Yanga
wanatengenezewa timu Aden anarahisisha anachukua wachezaji wazuri
anawapeleka Yanga ,Yanga leo hii wana Mrisho Ngassa,Emanuel okwi,Didier
Kavumbagu,Kiiza,Leo hii simba tunajua kabisa tunakwenda uwanjani tunajua
timu yetu ina mapungufu kiasi gani na umuongeze Emanuel Okwi pale’.
‘Naona Mwenyekiti hili ametutengenezea zile goli 5 zirudi au zaidi
nina mashaka nae,kwa sababu Manji alishawahi kutamka sisi tunajua kwamba
alisema kabisa nitapeleka kilio ndani ya timu ya Simba baada ya
kufungwa goli 5,na hili tunaliona msiba leo umetukuta wanachama wa Simba
na wapenzi wa Simba wote tuliokusanyika hapa toka asubuhi hii ni kwa
ajili ya suala la Emanuel Okwi,mwenyekiti wetu anatuchanganya kwa hili
na yeye ndo mhusika mkubwa kwenye suala hili’
‘Aden tunaomba atueleze kwa kina na mambo haya hawezi kutuambia sisi
kwenye vyombo vya habari kinachotakiwa suala Simba linazungumzwa na
wanachama wa Simba kwa sababu wanachama wa Simba ndio waliompa dhamana
Aden angoze Simba kinachotakiwa Aden awaitishie wanachama mkutano kama
alivyosema twende pale Police Mess twende tukajadili masuala kama haya
na ya aina mbalimbali Emanuel Okwi achukue winga pale na Mrisho Ngassa
na timu yetu sisi ina matatizo ina maana anataka goli hizi 5 zirudi
halafu yeye akikaa anawachukua watu 5 au 50 anachukua gari elfu 80
wanaenda Airpot wanampigia makofi akienda police mess anawaset watu
anaongea wanampigia makofi sisi hatuoni faida yoyote siye tunaipenda
club ya Simba sisi hatupendi Flemu za Simba sisi furaha yetu tunataka
nyavu zicheze,kama mzungu alivyotuambia pale Airpot hawa wote
waliokusanyika hapa wanataka furaha ndo maana wamenifata mimi’.
No comments: