Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam limetangaza kutoa donge nono la shilingi milioni 100/= kwa mtu
yeyote atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu
linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia na kuwadhuru watu kwa
tindikali.
Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman
Kova amesema: “Nimeamua kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe mtu
atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo
hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa.”
No comments: