Mfalme wa Saudi Arabia, ameingilia kati mpango wa
kumsaidia Raia wa nchi hiyo, Khalid bin Mohsen Shaari ambaye ndiye
binadamu mnene na mzito zaidi duniani akiwa na uzito wa kilogram 610,
katika mchakato wa kumtibu na kumrudisha
katika hali nzuri zaidi.
Kutokana na unene, ukubwa na uzito wake, Khalid hawezi kutembea wala
kusogea mwenyewe bila msaada wa kifaa maalum cha kumbeba akiwa katika
kitanda chake, na cha ajabu zaidi, Ni mshkaji mdogo tu ambaye umri wake
ni kati ya miaka 18 na
20.
Kwa mujibu wa rekodi za Guiness, Manuel Uribe kutoka Mexico ndiye
aliyekuwa akishikilia rekodi ya mtu mzito na mnene zaidi duniani ambapo
alikuwa na uzito wa kilo560, Na baada ya kuonekana na kuingizwa katika
matibabu, kwa sasa amepungua na kufikia uzito wa kilo 444.
Mfalme Abdullah tayari ametoa amri kuwa Khalid kuhamishwa huko Riyadh kwaajili ya mchakato wa matibabu yake.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/08/huyu-ndiye-binadamu-mwenye-kilo-610-na.html#ixzz2caceBCVR
No comments: