Chama cha Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ZANU -PF leo kimesema kimeibuka na ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi uliofanyika jana. Ushindi huo utamfanya Mugabe aiongeze nchi hiyo kwa miaka mitano mingine.
Hata hivyo mpinzani wake wa karibu amesema kura zimeibiwa.Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajia kutangazwa August 5. Chanzo kilicho karibu na Mugabe mwenye umri wa miaka 89, kimeiambia Reuters kuwa majibu yako wazi.
“Tumeshinda uchaguzi. Tumeizika MDC. Hatukuwa na mashaka yoyote kuhusu kushinda,” kilisema chanzo hicho.
Akijibu madai hayo, waziri mkuu nchi hiyo Morgan Tsvangirai ambaye ni mpinzani mkuu wa Mugabe kwenye uchaguzi huo, ameuelezea kama wa ulaghai. MDC kilipanga kuwa na mkutano wa dharura leo.
No comments: