Slider[Style1]

HABARI

BONGO MOVIES

BONGO FLEVA

.

BONGO VIDEOS

Style5[ImagesOnly]

STORY ZA INSTAGRAM



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu......Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.

Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.

About ujugu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

WHEAT CLICK THIS PHOTO