Boss wa Clouds FM Bw.Ruge Mutahaba katika maamuzi ya "hasira za mkizi"
*Ruge Mutahaba kashindwa kujibu shutuma za comando Lady Jay Dee.
*Wasanii hamkeni kujua nani mchawi wa kazi zenu.
Na Buberwa Jackob.
Watanzania leo tulikua tukimsikiliza mkurugenzi wa utafiti wa redio Clouds FM Bw.Ruge Mtahaba katika mahojiano na redio yake ya clouds fm, mahojiano ambayo tulikua tukitegemea boss Ruge ajibu shutuma dhidi yake za kumtilia kauzibe katika kupata riziki mwanamuziki Lady Jay Dee bint machozi, katika mahojiano hayo ambayo sisi wasikilizaji tunayafananisha sawa na KESI YA NYANI mwamuzi awe Ngedere.
Tulichokua tunakitegemea katika mahojiano ni majibu ya shutuma dhidi ya Bw.Ruge lakini cha kushangaza Ruge kashindwa kabisa kujibu shutuma zinazomkabiri baadala yake akawa anarusha rushua maneno na kuhusisha mifano ya wasanii walishuka na nani kapanda, na kuenda nje ya hoja ya msingi,mwisho wa mahojiano Bw.Ruge alikurupuka kwakauli za kuamrisha kuwa ni maarufu kupiga nyimbo za kizazi kipya (Bongo Fleva) kwa mda wa siku nzima katika kituo cha clouds fm.
Sasa watanzania tunajiuliza hivi redio ya Clouds FM au Redio ya Ruge na wasanii pamoja na sisi wanachi nani ? muhimu kwa karne hii ambayo taifa lina vituo vya redio zaidi ya 80?
Kwani wasanii wanamuhitaji sana Ruge na mshirika wake Bw.Kusaga,yaani wao ndio tuseme miungu ya wasanii?
Wananchi walio wengi wanamuunga mkono Lady Jay Dee kwa kutokukubali afanywe ngazi au kitendea kazi cha kuwanufaisha wanyonyaji katika soko la muziki,na kahamua kujitegemea.mahamuzi hayo ya Jay Dee ndio yanamfanya Jide atake kugeuzwa "Kondoo wa Sadaka" .
MRADI WA RUGE MTAHABA KATIKA SEKTA HII YA MUZIKI NI KUUA MUZIKI WA DANSI NA TAARABU NA KUJENGA MSINGI WA UTAMADUNI NA MZIKI WA KIZAZI KIPYA .
Ukisikiliza sana maelezo ya Ruge katika mahojiano utagundua wazi kuwa alijenga au alijaribu kujenga mtandao wa kuwamiliki na kuwajenga wanamuziki wa kizazi kipya kwa manufaa yake,yaani mwanamuziki hasipoingizwa katika mtandao huu basi hatojulikana na kazi zake azitotambulika ,yaani mtandao ambao pia unampendekeza msanii gani aukubalike kupewa tuzo hata kama si msanii mzuri, mtandao huu pia unatumika kama sululu la kuuchimbia kaburi muziki wa dansi na muziki wa taarabu,mtandao huu pia unawalazimisha watanzania walio wengi muziki gani wa kusikiliza, na mara nyingine kuwalazimisha wanamuziki nini cha kupiga( Beat) n.k.
Leo Ruge anapomsema Lady Jay Dee ampe kijiti mwingine na Lady Jay Dee anaposema yeye ni Lady Jay dee anapiga muziki kwa maisha yake na kuwalidhisha washabiki wake,hakuna haja ya kupokezana vijiti katika gemu la muziki. Bali mfumo huu kupokezana vijiti ni mfumo unaoitwa "Ruge Mtahaba System" na wasananii wamesha istukia kuwa si mfumo mzuri. Je ? wanamuziki wapo tayari kufanywa kete za kuchezea bao au chess! kwanini? lazima wasanii wapate pumuuzi ya uhai kutoka katika mtandao wa Ruge? hivi wasanii hawezi kusimama kidete na kuungana kwa pamoja wakajipigania na kukataa kufanya wapagazi katika sekta hii? Ruge kaonyesha Kiburi kwa kusema mziki wa bongo flava usipigwe kwa siku nzima redioni Clouds ! Sasa wasanii na nyinyi
Onyesheni mshikamano na msimamo wenu kwa Ruge,kuwa nanyi ni muhimu kwa jamii ya watanzania.
Je ? Nani mchawi wa kazi za wasanii na muziki wa Tanzania?
Watanzania na serikali ya Tanzania imeshuhudia kuangushwa kwa makusudi muziki wa dansi wa tanzania,
na kuchimbiwa kaburi utamaduni na sanaa za maonyesho wa watanzania,ujuma ambazo zinafanywa na mtandao ya siri ya wajanja wanaujumu utamaduni na muziki wa watanzania.
Na wanamtandao ambao wanaangaliwa macho bila ya kufanywa chochote na watanzania au kuchukuliwa hatua zozote na serikali kupitia idara husika.
Leo watanzania tunajiuliza hivi hawa akina Ruge Mtahaba wanazijua historia ya muziki wa Tanzania? na misingi ya miziki wa Tanzania, na wale waliojitoa waenga muhanga katika kujenga misingi hiyo imara? mbona nchi za wenzetu wanaendeleza misingi na miziki yao ya awali,kama ilivyo taarabu na mziki wa dansi.
Inakuaje leo hapa kuna baadhi ya wajanja wasiojua hata historia ya muziki wa tanzania watuchagulia nini? cha kusikiliza.
"JOTO HASIRA" KUNA HAJA YA KUWAFUKUZA KAZI NA KUVUNJA MTANDAO HUU UNAUJUMU UTAMADUNI ,MUZIKI NA WASANII WATANZANIA
No comments: