Slider[Style1]

HABARI

BONGO MOVIES

BONGO FLEVA

.

BONGO VIDEOS

Style5[ImagesOnly]

STORY ZA INSTAGRAM

Rais wa  jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amekatisha ziara yake nchini Kuwait na kurejea nchini kwa ajili kushughulikia tatizo la ulipuaji wa bomu iliyotokea Jiji la Arusha.
Mlipuko huo uliouwa mtu mmoja na kujeruhi wengine 62 ulitokea katika Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jijini hapo, mtu mmoja tayari anashilikiwa na Askari wa Jeshi la Polisi nchini kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.
Hatua ya Rais Kikwete kukatisha ziara yake nchini Kuwait imekuja siku moja baada ya kiongozi huyo kutoa kauli kali kwamba watuhumiwa wa tukio hilo nilazima watafutwe na kukamatwa mara moja.
“Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma. Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine”.
“Haiwezekani wahusika hao wawe na chimbuko lao ndani ama nje ya nchi yetu Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake”alisema Rais Kikwete akiwa nchini Kuwait.
Taarifa za Rais Kikwete kukatisha ziara yake nchini Kuwait zimelifikia mabovu story hivi punde kutoka vyanzo vya ndani katika idara ya Kurugenzi na Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam.

About ujugu

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

WHEAT CLICK THIS PHOTO